• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Waliofeli darasa la saba Nanyumbu watoa siri nzito

Posted on: January 2nd, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hamis H. Dambaya (mwenye miwani) pamoja na Kaimu Afisa Elimu Msingi Ndg. Nassa Mnonjela (wa pili kushoto waliokaa) wakiwa na wahitimu wa darasa la saba 2018 katika shule ya Msingi Nandembo


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hamis H. Dambaya amefanya mazungumzo na wahitimu wa darasa la saba (2018) wa Shule ya Msingi Nandembo pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Said D. Hassan ili kujua sababu ya wanafunzi wa shule hiyo kufeli kwa kiasi kikubwa na kupelekea shule hiyo kuwa ya mwisho kiwilaya na kimkoa.

Shule ya Msingi Nandembo ni miongoni mwa shule zenye historia ya kufanya vizuri katika Wilaya ya Nanyumbu ingawa katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 imejikuta ikiburuza mkia. Mwaka 2017 Nandembo ilifaulisha wanafunzi 50 wakiwemo wavulana 22 na wasichana 28 kati ya wanafunzi 78 waliofanya mtihani wa darasa la saba. Aidha, shule ilishika nafasi ya tano (5) kiwilaya kati ya shule 27 kutoka kundi lenye wanafunzi zaidi ya 40. Katika Matokeo ya mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 13 tuu, wakiwemo wavulana 9 na wasichana 4 walifaulu kati ya wanafunzi 67 waliofanya mtihani huo wakiwemo wavulana 28 na wasichana 39. Asilimia 80.6 ya watahiniwa hao wamefeli.

Wahitimu wa darasa la saba wakiwemo wale waliofaulu pamoja na waliofeli wameueleza uongozi wa Halmashauri namna walivyoagizwa na wazazi wao kuhakikisha wanafeli mtihani huo kwa kigezo kuwa wazazi hawaungi mkono watoto wao kwenda kusoma Shule ya Sekondari Lumesule kwani gharama za kupanga mtaani ni kubwa. Aidha, baadhi ya wazazi waliwaahidi watoto wao kuwa wakifeli watawapeleka gereji na vyuo vya cherehani. Pamoja na watoto hao kutekeleza maelekezo waliyopewa na wazazi wao, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kutotekelezewa ahadi walizoahidiwa na wazazi wao za kupelekwa vyuo vya cherehani na gereji na badala yake wamebaki  nyumbani kuendelea na shughuli za kilimo.

Ofisi ya Habari Nanyumbu ilizungumza na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandembo ambao waliwatupia lawama wenyeji wa kijiji cha Lumesule kuwa wamepandisha kodi za nyumba na kuwafanya watoto wao kuishi mazingira magumu huku idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha pili mpaka cha nne wakiwahamishia shule ya Sekondari Michiga ambayo ipo jirani na kijiji chao. Aidha, wahitimu wa darasa la saba 2018 Nandembo wakizungumza na Ofisi ya Habari, wameiomba Serikali kuwasaidia ili waweze kuendelea na masomo ili kutimiza ndoto zao.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu amelaani vikali tabia hii ya wazazi kuwarubuni watoto ili wafanye vibaya mitihani kwa kigezo cha kukwepa kuwasomesha. Aidha, amesema kuwa wazazi wengi na baadhi ya wanajamii  kwa maksudi hukwamisha maendeleo ya wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na kuwashawishi kuacha shule hali inayopelekea kuwa na idadi kubwa ya watoro shuleni. Uongozi wa Wilaya umeahidi kukomesha tabia hii ili kuinua kiwango cha Elimu wilayani Nanyumbu.  






Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.