• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Complaints |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • List of Leaders
    • Dira na Dhamira
    • Core Values
    • Stategies
  • Administration
    • Muundo
    • Idara
      • Water
      • Kilimo
      • Finance and Accountants
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Historia

1. UTANGULIZI 

1.1 TASWIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU

Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, ni moja kati ya Halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara. Halmashauri hii ilianzishwa chini ya Sheria namba 7 ya mwaka 1982 ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na kutangazwa rasmi katika Gazeti la Serikali Na. 190 la tarehe 01 Julai 2007. Makao makuu ya Wilaya yapo mji wa Mangaka ambao upo umbali wa kilomita 54 kutoka Masasi kwenye barabara ya Mtwara-Songea.

Asili ya wenyeji wa wilaya ya Nanyumbu ni makabila ya wamakua, wayao, na wamatambwe ambao huzungumza lugha zao za asili pamoja na Kiswahili.

1.2 MIPAKA YA ENEO

Wilaya hii iko kati ya latitudo 360 na 380 mashariki mwa Greenwich na latitudo 100 na 120 kusini mwa Ikweta. Nanyumbu inapakana na wilaya ya Nachingwea upande wa kaskazini, wilaya ya Masasi kwa upande wa mashariki, wilaya ya Tunduru upande wa magharibi na Jamhuri ya Msumbiji kwa upande wa kusini.

1.3 HALI YA HEWA

Hali ya hewa katika wilaya ya Nanyumbu ni joto la wastani ambalo ni 25 0C huku joto la juu likiwa 32 0C. Kipindi cha Desemba hadi Aprili, upepo unaojaa unyevunyevu kutoka Kaskazini-Mashariki huelekea Kusini Magharibi na kupelekea msimu wa mvua wenye joto na unyevunyevu. Aidha, kipindi cha Mei hadi Novemba, upepo kutoka Kusini Mashariki husababisha wilaya kuwa kavu, baridi na isiyo na unyevunyevu. Wilaya hupata mvua ya  wastani wa 832 mm ambayo hunyesha msimu mmoja kwa mwaka kuanzia mwezi Desemba hadi Aprili.

1.4 ENEO LA KIUTAWALA

Wilaya ya Nanyumbu ina tarafa nne za kiutawala ambazo ni Nakopi, Nanyumbu, Mangaka na Maratani pamoja na jimbo moja la uchaguzi (Jimbo la Nanyumbu). Wilaya imegawanywa katika kata 17, vijiji 93 vilivyosajiliwa na vijiji vidogo 526. Wilaya ya Nanyumbu ni kubwa kijiografia ikilinganishwa na halmashauri zingine za mkoa wa Mtwara kwani ina eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 5,071.5. Ukubwa wake wa kijiografia ni asilimia 30 ya Mkoa mzima ambao una eneo la ardhi la kilomita za mraba 16,720.

Ugawaji wa eneo la ardhi katika wilaya ya Nanyumbu unaonesha kuwa, tarafa ya Nakopi inachukua sehemu kubwa ya eneo la ardhi ikiwa na kilomita za mraba 1665.7, ikifuatiwa na tarafa ya Nanyumbu yenye kilomita za mraba 1628. Tarafa ya Mangaka ina kilomita za mraba 1040.4 huku tarafa ya Maratani ina eneo la jumla ya kilomita 737.4 za mraba.

1.5 IDADI YA WATU

Kwa Mjibu wa Sensa ya Kitaifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, wilaya ilikuwa na jumla ya wakazi wapatao 150,857 ambao ni wanawake 72,237 na wanaume 78,620. Ongezeko la watu ni wastani wa asilimia 2.1 kwa mwaka. Pato la mwananchi wa Wilaya ya Nanyumbu linakadiriwa kuwa Tshs 442,572 kwa mwaka.

1.6 SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Wilaya ya Nanyumbu hujishughulisha na shughuli za kilimo kwa ajili ya chakula na biashara. Mazao ya biashara yanayolimwa ni korosho, ufuta, karanga, choroko na mbaazi. Mazao ya chakula ni mahindi, mpunga, muhogo, mtama, mbaazi, njugumawe, kunde na upupu. Aidha, baadhi ya wakazi hujishughulisha na uvuvi katika mto Ruvuma.

Matangazo

  • Tangazo la Kazi za Muda za MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 May 06, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU July 02, 2022
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Mtwara waadhimisha Wiki ya Maji Nanyumbu

    March 24, 2023
  • Miaka miwili ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan

    March 17, 2023
  • Serikali yaendelea kujenga barabara za lami wilayani Nanyumbu

    March 14, 2023
  • DED Mwanauta awakumbusha watumishi Nanyumbu kutimiza wajibu

    March 10, 2023
  • Ona yote

Video

Utalii wa ndani Nanyumbu
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • miongozo

Tovuti Mashuhuri

  • Public Service Management
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.