• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

KAMATI YA PHC NANYUMBU YAJADILI MLIPUKO WA KIPINDUPINDU NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAO.

Posted on: October 28th, 2025

Na; Airin Lipuka

Kamati ya Huduma za Afya ya Msingi (PHC) Wilaya ya Nanyumbu, chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mheshimiwa Christopher E. Magala, imekutana leo tarehe 27 Novemba 2025 katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mangaka kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kuathiri baadhi ya vijiji wilayani nanyumbu..

Katika kikao hicho, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mangaka, Ndugu Marco J. Mazanzagar, aliwasilisha taarifa rasmi ya mlipuko huo kwa kamati. Akieleza hali ya ugonjwa huo, alisema:

“Ugonjwa wa kipindupindu uligundulika tarehe 12 Oktoba 2025 katika kitongoji cha Sauti Moja, kijiji cha Chitowe, na baadaye kusambaa hadi maeneo ya Mangaka na Kilimanihewa. Hadi sasa, jumla ya wagonjwa 20 wamethibitishwa kuambukizwa, huku kifo kimoja kikiripotiwa. Vijiji vilivyoathirika ni Chitowe, Mangaka, Kilimanihewa, Kazamoyo, Masyalele na Mkohora. Chanzo kikuu cha maambukizi ni matumizi ya maji yasiyo safi na salama.”


Katika mjadala uliofuatia, Afisa Mazingira wa Wilaya ya Nanyumbu, Ndugu Elias Matandiko, aliongeza kuwa sababu nyingine inayochangia kuenea kwa ugonjwa huo ni ukosefu wa vyoo katika baadhi ya kaya, hali inayowalazimu wakazi kutumia vichaka kama mbadala wa vyoo. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na maafisa wa afya wanapotoa elimu na kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi.

Kamati hiyo iliweka mikakati kadhaa ya kukabiliana na mlipuko huo, ikiwemo:

  • Kuendelea kutoa elimu ya afya mashuleni na katika sehemu za ibada
  • Kuendelea kuendesha mikutano ya kijamii na kampeni za uhamasishaji kuhusu kipindupindu
  • Kutoa matangazo ya mara kwa mara kuhusu tahadhari na hatua za kujikinga

Akihitimisha kikao hicho, Mwenyekiti Mheshimiwa Christopher E. Magala nalitoa wito kwa taasisi husika kuchukua hatua za haraka:

“Nasisitiza umuhimu wa usafi binafsi na usafi wa mazingira. Nawaagiza RUWASA kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, kwani hilo ndilo chanzo kikuu cha mlipuko huu. Elimu kwa wananchi ni silaha muhimu katika kuzuia maambukizi zaidi.”

Kikao hicho kilifungwa rasmi baada ya majadiliano ya kina na kuweka mikakati ya utekelezaji wa haraka.

Matangazo

  • Tangazo la Kuhudhuri Mafunzo ya Uchaguzi Jimbo la Nanyumbu October 21, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • KAMATI YA PHC NANYUMBU YAJADILI MLIPUKO WA KIPINDUPINDU NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAO.

    October 28, 2025
  • Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura Nanyumbu Wapigwa Msasa Kuelekea Oktoba 29

    October 26, 2025
  • Makarani Waongozaji Wapiga Kura Nanyumbu Waaswa Kutekeleza Majukumu kwa Uadilifu

    October 25, 2025
  • Vyombo vya Ulinzi na Usalama Vyaendesha Mazoezi ya Pamoja Nanyumbu

    October 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.