• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

MHE. SAWALA AWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA WATOTO WENYE SIFA WARIPOTI SHULENi.

Posted on: January 16th, 2026


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wenye sifa za kujiunga na shule wanaripoti kwa wakati, bila kujali ukosefu wa sare au vifaa vingine vya shule. Amesisitiza kuwa mtoto anaweza kuanza masomo mara moja huku mahitaji mengine yakiendelea kufuatiliwa akiwa shuleni.

Mhe. Sawala ametoa wito huo tarehe 15 Januari 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, iliyolenga kukagua miundombinu ya elimu na hali ya uripoti wa wanafunzi. Akiwa katika Shule ya Msingi Lidede, iliyopo Kijiji cha Lidede, Kata ya Kilimanihewa, Mkuu wa Mkoa aliwahimiza wazazi kushirikiana na walimu na viongozi wa shule katika kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo kikamilifu.

Katika ziara hiyo, Mhe. Sawala aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lidede kwa ushirikiano wao mzuri katika ujenzi wa miundombinu ya shule, na kuwataka waendelee kuunga mkono jitihada za walimu hususan katika suala la lishe shuleni, kwa lengo la kupunguza utoro na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Aidha, aliwataka viongozi  kuongeza jitihada, ikiwemo kutumia mbinu mbadala pale inapobidi, ili kuhakikisha ujenzi wa mradi wa shule unakamilika kabla ya tarehe 31 Januari 2026.

Ujenzi wa mradi  katika Shule ya Msingi Lidede unahusisha madarasa manne, ofisi moja ya walimu na matundu tisa ya vyoo. Mradi ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 12/9/2025 mara baada yakupokea fedha kiasi cha  shilingi 112,401,789.99 kutoka Serikalini kupitia Mpango wa BOOST huku wananchi wakishiriki katika shughuli ndogondogo katika kukamilisha mradi huo.

Wazazi wameshukuru sana Serikali kwa jitihada hizo, wameeleza kuwa Ujenzi wa Shule ya Msingi Lidede Umeondoa Msongamano wa Wanafunzi katika shule mama ya Kilimanihewa na Umbali wa Kutembea kwa wanafunzi.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA November 26, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • MHE. SAWALA AWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA WATOTO WENYE SIFA WARIPOTI SHULENi.

    January 16, 2026
  • WATUMISHI TARAFA YA NANYUMBU WAFURAHIA UTALII WA NDANI LUKWIKA–LUMESULE.

    December 08, 2025
  • UZIDUZI WA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA NANYUMBU WAFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU.

    December 02, 2025
  • KAMATI YA PHC NANYUMBU YAJADILI MLIPUKO WA KIPINDUPINDU NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAO.

    October 28, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.