Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Marium Chaurembo (wa tatu kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maneme
Na, Lunanilo Ngela
Mhandisi Samweli Bundala wa Wizara ya Elimu pamoja na msanifu majengo ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Ndg. Dotto Saganda wamemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Marium Chaurembo pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo kuwa Serikali itatekeleza ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi katika kijiji cha Maneme.
Akizungumza katika eneo lililotengwa kijijini hapo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo hicho, Mhandisi Bundala amesema kuwa eneo lililotengwa linafaa kwa ujenzi huo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu amesema kuwa ujezi wa chuo hicho umekuwa shauku kubwa kwa wananchi hao ambao kwa moyo wa dhati wametenga ekari 40 ili kuwezesha ujenzi wa chuo hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Benjamini Masimbo, Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Salum Palango pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Philipo Sengela wameishukuru Serikali kwa kudhamiria kujenga chuo hicho wilayani Nanyumbu.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.