" Tumehitimisha MAADHIMISHO ya Muungano kwa Bonanza la NANYUMBU Derby "
• CRDB na Mhe.Mbunge waunga mkono.
Wilaya ya Nanyumbu kama maeneo mbalimbali ya Nchi nayo imeadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Taifa la Tanzania kwa namna ya kipekee.
Shughuli zilizofanyika zilikuwa ni pamoja na usafi wa mazingira katika Kata zote za Wilaya ya Nanyumbu, ambapo katika ngazi ya Wilaya usafi ulifanyika katika Hospital ya Mangaka.
Aidha, mchana ulifanyika mdahalo katika Jengo la Halmashauri ambapo watoa mada mahiri waliwasilisha ili kuwarithisha Vijana wetu wa Shule za SEKONDARI tunu hii muhimu.
Mwisho, Jioni tulimaliza na Mechi kabambe ya WAPINZANI wa jadi
" Nanyumbu Derby " Kati ya Kata za Mangaka na Kilimanihewa ambapo Kata ya Kilimanihewa waliibuka kidedea kwa Ushindi wa Goli 2-1 na kujinyanyukulia Zawadi nono iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Pia ilitumika nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kushiriki katika Sensa ya sita (6) ya Watu na makazi toka Muungano ambayo itafanyika mwezi Agosti 2022.
Shughuli hizo zote ushiriki wa Chama cha Mapinduzi ulikuwepo ambapo KATIBU wa CCM Wilaya Ndg. Eliud Shemauya aliongoza Jahazi.
Shukrani za dhati kwa wadhamini wetu wa mpambano huo ambao ni Benki ya CRDB Tawi la Nanyumbu na Mhe.Yahaya Ally Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu kwa kuzipatia Timu zote maji yakutosha kabla na wakati wote wa Mchezo.
na mwandishi wetu S.Palango
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.