• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Serikali kushughulikia soko la Korosho

Posted on: October 29th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Machali (wa kwanza kulia) akiwa katika Mkutano na wananchi wa Mji wa Mangaka uliofanyika Jana Tarehe 28/10/2018 Mangaka Mjini


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu amekutana na wananchi wa Mji wa Mangaka na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu soko la korosho katika Msimu huu wa kilimo wa 2018/2019. Akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Magufuli anawaunga mkono wakulima kwa kukataa bei ndogo ya korosho. Aidha, amesema kuwa nia na lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima anapata soko zuri la uhakika. Wananchi wameshauriwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kifupi wakati Serikali inashughulikia soko la Korosho.

Mheshimiwa Machali pamoja na kuzungumzia soko la Korosho pia ameviagiza vyama vyote vya Msingi vya ushirika vinavyodaiwa fedha za wakulima katika msimu uliopita wa 2017/2018 kuhakikisha vinalipa fedha hizo kabla ya Mwezi Disemba mwaka huu.

Akizungumzia suala la usafi wa mazingira, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapongeza wananchi kwa kufanikiwa kuufanya Mji wa Mangaka kuwa safi. Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya watu wenye mifugo mfano mbuzi na ng'ombe kuiacha mifugo hiyo ikizurura mtaani na kuchafua mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Mkuu wa Wilaya ameagiza watu wote wanaoiacha mifugo ikizurura mjini wachukuliwe hatua.

Wananchi wamesisitizwa kulima Ufuta na alizeti na kutotegemea Korosho peke yake kama zao la biashara. Aidha, Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Idara ya Kilimo Nanyumbu inafanyia utafiti zao la mhogo. Mkuu wa Wilaya pia amewashauri wafanya biashara wa Wilaya ya Nanyumbu kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo mfano vya kukamua mafuta ya alizeti ili kuongeza kipato.

Akizungumzia suala la maji, Mheshimiwa Machali amesema kuwa Wilaya inaendelea kuchimba visima ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kusanifu mabwawa sita (6) yatakayosambaza maji kwa wananchi. Aidha, kufanikiwa kwa mradi huo mkubwa wa mabwawa kutategemea upatikanaji wa fedha.

Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu waliozungumza na Ofisi ya Habari wamemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr, John Pombe Magufuli kwa kusima kidete katika kutetea wakulima na wananchi wanyonge. Aidha, wametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu kwa kujitoa mhanga kutetea  wakulima na wananchi kwa ujumla.




Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.