" LORI la KIMKAKATI "
Aliyewahi kuwa Bingwa wa Uzito wa Juu wa Masumbwi Dunia Muhammad Ally alipata kusema,
" Champions aren't made in the Gym.
Champions are made from something they have deep inside them - a desire, a dream and a vision "
Akimaanisha, washindi hawatengenezwi katika Nyumba za mazoezi ( Gym) bali kwa kile wanachoamini sana ndani ya maono yao, ndoto yao na matamanio yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imenunua Lori la KIMKAKATI kuhakikisha inaongeza mapato na kuongeza kasi ya ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Nanyumbu.
Lori hilo lenye namba za usajili SM 14500 na uwezo wa kubeba Tani 14 limenunuliwa kwa thamani ya Tsh.Milioni 140 fedha za mapato ya ndani.
Itakumbukwa Kuwa, Wilaya ya Nanyumbu ina Mradi wa ufyatuaji wa TOFARI ambazo zina ubora uliothibitishwa maabara na kutumika katika miradi mbalimbali ya Halmashauri na Watu binafsi.
Hivyo, ununuzi wa Lori hilo litachochea zaidi ukuaji wa Biashara ya usambazaji wa TOFARI, mchanga, Kokoto, saruji n.k na hivyo kuongeza Mapato ya Halmashauri na ajira kwa Vijana na kusaidia kuongeza nguvu ya Halmashauri katika kuwahudumia Wananchi.
Uzinduzi rasmi wa matumizi ya Lori hilo ulifanywa Tarehe 25/03/2022 na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Mariam Khatibu Chaurembo na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Comred Benjamin Masimbo.
Hongera Watendaji wa Halmashauri ya Nanyumbu chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Ibrahim Mwanauta na Baraza la Waheshimiwa Madiwani kwa maamuzi mazuri ya kimkakati.
" Acha Kazi iendelee "
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.