• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Nanyumbu yafanya mapinduzi makubwa sekta ya kielimu

Posted on: July 5th, 2018

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mangaka akionesha namna ya kutumia kompyuta katika matumizi mbalimbali mbele ya wazazi na wageni waalikwa waliohudhuria kilele cha Juma la Elimu kiwilaya

Juma la Elimu wilayani Nanyumbu limekamila katika viwanja vya Shule ya Msingi Kilimanihewa huku wadau mbalimbali wa Elimu wakipongeza hatua mbalimbali ambazo Wilaya ya Nanyumbu imefanya ili kuboresha Elimu.  Wilaya ya Nanyumbu ina shule za msingi tisini na nne (94) na shule za sekondari kumi na mbili (12). Aidha, kuna jumla ya wanafunzi 39,608 wa shule za Msingi na wanafunzi 3,572 wa shule za sekondari. Wilaya ina jumla ya walimu 608 wa Shule za Msingi na walimu  226 wa Shule za Sekondari.

Wilaya ya Nanyumbu ikishirikiana na wananchi imefanya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule ili kuhakikisha kiwango cha Elimu kinaongezeka. Mwaka 2017/2018 Nanyumbu imefanya ujenzi wa madarasa 146, nyumba za walimu 46, matundu ya vyoo 192, Ofisi za walimu 15. Aidha, ukarabati wa maabara za sayansi na ujenzi wa hosteli unaendelea kwa shule mbalimbali za Sekondari. Ujenzi wa miundombinu hiyo umekamilika kwa baadhi ya shule.

Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu, Seifu Chilumba akisoma risala kwa Mgeni rasmi amesema kuwa, Wilaya ya Nanyumbu pamoja na kwenda kwa kasi katika ujenzi wa miundombinu ili kumaliza kabisa tatizo la ukosefu wa miundombinu ya shule pia Wilaya imepata mafanikio katika maeneo mengine ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha wanafunzi wengi zaidi wa madarasa ya awali na darasa la kwanza ikilinganishwa na miaka iliyopita, kupunguza utoro na hasa kwa shule za Sekondari, kuongeza ufaulu kwa shule za msingi na Sekondari ikilinganishwa na miaka iliyopita. Mwaka 2017 Hali ya ufaulu kwa shule za msingi imeongezeka na kufikia asilimia 51.48 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo ufaulu ilikuwa ni asilimia 32 tu. Aidha, Ufaulu umeongezeka kwa Shule za sekondari katika mwaka 2017 na kufikia asilimia 77 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo ufaulu ilikuwa asilimia 56.5.

Wazazi na wadau wa Elimu wametowa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mh.Selemani Mzee, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu Ndugu Hamis H. Dambaya, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mh. Dua W. Nkurua, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Salum A. Palango pamoja na watendaji wengine katika ngazi mbalimbali kwa kuhakikisha wanainua kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Nanyumbu. Wananchi wamesema pia katika kipindi cha mwaka 2016/2017 na 2017/2018 wameiona kasi kubwa ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikilinganishwa na miaka iliyopita. Aidha, wananchi wamempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa kuwasimamia vizuri watendaji wote wa Serikali ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aidha, Wananchi wamekiri kuwa sasa wanaiona Tanzania mpya ya wachapakazi.

Juma la elimu kwa mwaka 2018 limeongozwa na Kauli mbiu isemayo ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA, WEKEZA SASA.


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.