• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Nanyumbu wahamasishwa kutoa maoni Dira ya Taifa ya Maendeelo 2050

Posted on: July 23rd, 2024

Na, Lunanilo Ngela

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Mangaka, Ndg. Baraka Mlahagwa, ameongoza kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Wilaya kilichofanyika Julai 23, 2024, kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na matarajio ya Dira mpya ya Maendeleo 2050.

Kikao hicho, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, kilihudhuriwa na wajumbe pamoja na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wadau, ikiwemo sekta binafsi, asasi za kiraia, taasisi za dini, na makundi maalum kama vijana, wanawake, wazee, wakulima, wavuvi, wasafirishaji, watu wenye mahitaji maalum, vyama vya michezo na sanaa, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wafugaji, wafanyabiashara ndogondogo, vyama vya ushirika, na vyama vya wafanyakazi.

Mwenyekiti wa kikao hicho aliwaeleza wajumbe kuwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ilizinduliwa mwaka 1999 na Serikali ya Tanzania, ikilenga kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kuboresha miundombinu na huduma za kijamii kama vile elimu, afya, na upatikanaji wa maji safi, kuongeza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria, na haki za binadamu pamoja na kujenga uchumi unaoongozwa na viwanda ili kuongeza ajira na kipato cha wananchi.

Washiriki wa kikao hicho walielezea mafanikio mbalimbali ya utekelezaji wa Dira ya 2025, ikiwemo Tanzania kuingia katika kundi la nchi za kipato cha kati, kuimarika kwa huduma za elimu, afya, miundombinu ya usafiri, mawasiliano, umeme, maji safi, na usawa wa kijinsia hususani kwenye elimu na nafasi za uongozi.

Wananchi hao walisema kuwa Dira ya Maendeleo 2050 ilenge kumaliza tatizo la ajira kwa vijana, kuimarisha sekta za viwanda na madini ili kuondoa utegemezi kwa mataifa yaliyoendelea, na kuwawezesha wakulima wadogo kutumia zana bora za kilimo badala ya jembe la mkono na kutegemea mvua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ndg. Ibrahim Mwanauta, alisisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi hawaachwi nyuma katika mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na hivyo kuwasihi watu wote kutoa maoni yao kwa njia ya simu kwa kuingia *152*00# au kwa kujaza dodoso lililopo mtandaoni kupitia https://dira2050portal.planning.go.tz/tume/dira 

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.