Na mwandishi Baraka Mlahagwa - Kaimu Katibu Tawala Wilaya.
Historia inaenda kuandikwa !
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu *Mhe Mariam Khatibu Chaurembo* Leo tarehe 06/05/2022 amewatembelea wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Mangaka na kufanya nao kikao kifupi. Mkuu wa Wilaya, amewatia moyo wanafunzi hao na kuwahasa kutumia muda wao vizuri kwa maombi na Sala katika Kuelekea kufanya Mitihani yao ya Mwisho itakayoanza wiki ijayo.
Aidha amewataka ku _focus_ zaidi kwenye Mitihani yao kwa kuendelea kujisomea hasa kwa kufanya _groups discussions_ ili kuwa na uelewa wa pamoja na kutenga muda wa kupumzika
Itakumbukwa kuwa Nanyumbu inaenda kutoa Wanafunzi wa kidato Cha sita kwa Mara ya kwanza *toka Nchi yetu ipate Uhuru*, hivyo kufanya kwao vizuri katika Mitihani hiyo kutaongeza chachu ya kusoma kwa bidii kwa Wanafunzi wa Kidato cha tano wanaobaki na itaonyesha dira njema kwa maeneo mengine ya Wilaya ya Nanyumbu hasa kwa shule zilizowekwa kwenye Mpango wa Kidato cha 5 & 6 hapo baadae.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.