• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Nanyumbu kuadhimisha Siku ya Elimu kiwilaya

Posted on: January 5th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali akizungumza na washiriki wa Siku ya Elimu wilayani Nanyumbu iliyofanyika Tarehe 05/Jan/2019


Na, Lunanilo L. Ngela

Wadau wa Elimu katika Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali wamekutana mapema leo Januari 05, 2018 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mangaka katika kuadhimisha siku ya Elimu kiwilaya. Miongoni mwa washiriki katika siku hii mhimu kielimu ni pamoja na Mhe. Dua W. Nkurua (Mb), Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Uongozi wa CCM (W), Wakuu wa Idara na Vitengo, Waratibu Elimu Kata, Watendaji wa Kata na Vijiji, Viongozi wa Bodi za Shule, Wadau mbalimbali wa Elimu, Walimu, Wazazi na Wanafunzi.

Uongozi wa Wilaya ya Nanyumbu umeamua kuiteua siku hii, ili kupokea Taarifa mbalimbali za Elimu Msingi na Sekondari, Taarifa ya Mthibiti Ubora wa Shule, Kujadili kwa kina hali ya Elimu na mwelekeo kwa mwaka 2019 ikiwa ni pamoja na ugawaji Tuzo. Siku ya Elimu iliasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Gasper Byakanwa ambaye alizitaka Wilaya zote kufanya Tathmini ya hali ya Elimu kila mwaka ili kubaini kama Wilaya inapanda au inashuka ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki  

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akizungumza katika maadhimisho hayo amewataka watumishi wote katika Sekta ya Elimu kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu huku wakitanguliza mbele maslahi ya umma. Mhe. Machali amelaani vikali tabia ya wazazi kuwashawishi watoto kujifelisha katika mitihani ili kukwepa jukumu la kuwasomesha. Mkuu wa Wilaya amewakumbusha wananchi kushiriki shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule, kuwapatia watoto chakula, kudhibiti utoro na uzembe kwa wanafunzi, kushughulikia maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha walimu wanakuwa na maandalio ya masomo pamoja na zana zote mhimu za kufundisha na kujifunzia.

Pamoja na Changamoto mbalimbali ikiwepo uhaba mkubwa wa walimu, Wilaya ya Nanyumbu imeendelea kupanda mwaka hadi mwaka katika matokeo ya darasa la saba. Mwaka 2016 kulikuwa na asilimia 32.53 ya wanafunzi waliofaulu huku asilimia hiyo ikipanda mwaka 2017 ambapo wanafunzi walifaulu kwa asilimia 51.48 na kupanda zaidi mwaka 2018 ambapo ufaulu  ulifika asilimia 72.22.

Wadau mbalimbali waliohudhuria Siku ya Elimu wilayani Nanyumbu walitoa ushauri na maoni mbalimbali ya namna ya kuinua kiwango cha Elimu Wilayani Nanyumbu. Pamoja na maoni hayo pia wadau hao wa Elimu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu wamekusudia kufanya mapinduzi makubwa ya kielimu ili kuhakikisha Nanyumbu inakuwa mfano bora wa kuigwa kielimu.


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Mradi wa Maji Mto Ruvuma, DC Magala Atoa Maagizo Mazito

    July 11, 2025
  • Nanyumbu Yatikisa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025

    July 10, 2025
  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.