SHUKRANI
" Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "
Ndugu zangu ni mwaka mmoja sasa toka *Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania* aniteue na kunipa dhamana ya kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
kipekee na thamini sana ushirikiano munaonipa katika kutekeleza majukumu yangu, nawaomba muendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuliendeleza gurudumu la maendeleo la wilaya yetu.Hakika kila mmoja wenu amekuwa kiungo muhimu katika kutimiza vyema Majukumu yangu.
Nikishukuru Chama changu cha Mapinduzi, Kamati ya ULINZI na Usalama, Mhe.Mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani wote,Wakuu wa Idara,Taasisi zote,Maafisa Tarafa na Watendaji wote wa Serikali wa ngazi zote.
Mwisho, ila siyo kwa umuhimu, nikushukuru DAS wangu kwa ushirikiano unaonipa nakuombea kwa Mungu sana azidi kukupa Hekima, BUSARA & Afya njema ya kuendelea kukupa nguvu ya kuzidi kuchapa kazi.
Wewe ni mtu mwema sana kwangu na Wilaya kwa ujumla.Nikutie moyo na Hali ya kufanya Kazi kwa bidii na kumtanguliza Mungu kila uchwao leo.
Nawashukuru sana na Kazi iendelee
Mariam K. Chaurembo
MKUU wa Wilaya NANYUMBU
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.