• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mpango wa TASAF waja na matokeo chanya Nanyumbu

Posted on: July 7th, 2024

Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Christian Mchopha (wa tatu kulia) akizungumza na wanufaika wa Mpango wa TASAF

Na, Lunanilo Ngela

Wanufaika wa Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wilaya ya Nanyumbu wametoa shukrani zao za dhati kwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wakielezea matokeo chanya waliyopata kwenye mpango huo wa kitaifa ulioanzishwa mwaka 2000 na Serikali.

Wakizungumza Julai 05, 2024 wakati wakipokea fedha za Mpango za mwezi Machi na Aprili katika bajeti ya 2023/2024, kiasi cha shilingi milioni 377.6, wanufaika hao walisema kuwa mpango huo umekuwa nguzo muhimu katika kuboresha maisha yao na kuwawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Bi. Awetu Alfani wa Kijiji cha Mnanje B alisema “Fedha niliyopewa nilitumia kununua kuku watano na kuanza safari ya ufugaji. Nilifanikiwa kuwa na kuku 250.” aliongeza kuwa aliuza baadhi ya kuku na kununua bati na kuezekea nyumba anayoishi sasa kwani hapo awali alikuwa anaishi kwenye nyumba ya nyasi.

Mnufaika mwingine, Bi. Mwajuma Athumani wa Mnanje A, alieleza kuwa alipata shilingi laki tatu na nusu kutoka ruzuku ya uzalishaji zilizomwezesha kujenga banda la kuku na kuanza ufugaji. "Nilianza na kuku 12 na sasa nina kuku 46. Ufugaji wa kuku umekuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa familia yangu, huniwezesha kusomesha watoto na kumudu gharama za maisha," alieleza Bi. Mwajuma.

Naye Bi. Mwanahawa Mkane wa Mnanje B, mnufaika wa mpango huo, alisema kuwa fedha alizopata kutoka TASAF zimemwezesha kuanzisha ufugaji wa bata na kuku. Pia, fedha hizo zimemsaidia kununua chakula na kugharamia matibabu. "Nimenunua redio pia ili niwe nasikiliza taarifa za habari," aliongeza Bi. Mwanahawa.

TASAF imekuwa mkombozi kwa wananchi wenye kipato cha chini Wilaya ya Nanyumbu. Mpango huo umesaidia kuboresha maisha ya walengwa kwa kuwawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile ufugaji, kilimo, na biashara ndogo ndogo. Kupitia Mpango huo, wanufaika wana matumaini mapya ya kujitegemea kiuchumi.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili June 11, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • RC Sawala Apongeza Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kilimanihewa, Awataka Wananchi Kuendeleza Ushirikiano

    June 11, 2025
  • DC Magala Afungua Mafunzo ya Jeshi la Akiba Nanyumbu

    June 10, 2025
  • "Tutachukua Hatua Kali kwa Watakaohujumu Wakulima" DC Magala

    June 09, 2025
  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.