Na, Lunanilo Ngela
Mahakama ya Wilaya Nanyumbu mkoani Mtwara, imemhukumu Defao Kashimu Abdallah (26) mkazi wa Kijiji cha Likokona kitongoji cha Mkwajuni kwenda jela miaka 60 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka na kumlawiti binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka tisa (Jina linahifadhiwa).
Defao aliyehukumiwa Agosti 28, 2023 na Mahakama ya Wilaya alitenda kosa hilo la kumbaka na kumlawiti mtoto huyo na kisha kumpiga jambo lililopelekea majirani kuingilia kati sakata hilo.
Makundi mbalimbali ya wananchi wakizungumzia sakata hilo, wametowa shukrani kwa Mahakama ya Wilaya, Jeshi la Polisi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kwa kuhakikisha haki inatendeka.
Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ni hatua mhimu katika kukomesha vitendo vya ubakaji na ulawiti ambavyo vipo maeneo mengi huku wakiinyoshea kidole zaidi kata ya Nangomba.
Jeshi la Polisi Wilaya Nanyumbu pamoja na Maafisa Ustawi wa Wilaya wameeleza namna wanavyopambana na matukio hayo na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi ukatili wa jinsi hiyo unapotokea.
Aidha, wameeleza pia kuwa wazazi wengi na mashuhuda wa matukio hayo hukataa kutoa ushirikiano pindi wanapohojiwa na kufanya kesi hizo kuchelewa kufikia maamuzi na hivyo kuwasihi wananchi kishirikiana na vyombo vya dola ili kufanikisha upatikana wa suluhu ya mashauri hayo mahakamani.
Katika ripoti iliyowasilishwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kiwilaya ilifanyika Shule ya Sekondari Mangaka mwaka huu, inaonesha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu (Januari – Machi 2023) jumla ya watoto 248 walipata mimba za utotoni, idadi hiyo inajumuisha wanafunzi na watoto wasiosoma wenye umri chini ya miaka 18.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.