Na; Lunanilo Ngela
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali. Ahmed Abbas Ahmed ametowa pongezi za dhati kwa viongozi na wananchi wa Wilaya ya Nayumbu kwa kutekeleza miradi bora ya maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu na Afya.
Pongezi hizo amezitowa mapema Oktoba 30, 2023 alipotembelea Wilaya hiyo kwa ziara ya siku moja, akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Shule mpya ya Msingi na Awali Kilimanihewa inayogharimu shilingi Milioni 608.2 kupitia mradi wa BOOST.
Miradi mingine aliyoikagua ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Kitaifa ya wasichana eneo la Naishero Kata ya Mangaka, inayogharimu shilingi Bilioni 3 toka Serikali Kuu, ujenzi wa Zahanati ya Lukula iliyopo Kata ya Masuguru, ujenzi wa Barabara ya Bomani – Mangaka Nachingwea boarder pamoja na Mradi wa maji wa mto Ruvuma.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa, ameridhishwa na hatua za ujenzi wa miundombinu hiyo hususani miradi ya Elimu na kutoa rai kwa mafundi pamoja na watendaji ngazi ya Wilaya kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili kupokea wanafunzi wa shule za Awali, Msingi na Sekonadari ifikapo Januari 2024.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo akizungumza katika ziara hiyo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya hiyo miradi mingi ya maendeleo. Aidha, ameahidi kuwa kwa kushirikiana na watendaji wengine wa Wilaya pamoja na wananchi watakamilisha ujenzi wa muindombinu hiyo kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.