• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu apongezwa na Halmashauri kuu ya CCM Wilaya

Posted on: March 4th, 2020

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Willium Nkurua akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi Cha 2015-2020


Na, Lunanilo L. Ngela

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Rashidi Ally Mrope wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Dua William Nkurua kwa kutekeleza vema majukumu yake ya Ubunge. Wajumbe hao wametoa pongezi hizo baada ya Mbunge huyo kuwasilisha taarifa yake ya Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi Cha 2015-2020.

Katika taarifa hiyo Mhe. Dua pamoja na kuhamasisha Maendeleo jimboni kwake amepambana kuhakikisha anapata fedha za Miradi ya Maendeleo kupitia Wizara mbalimbali ambapo Nanyumbu imeingiziwa Fedha za upanuzi wa Miradi ya Maji Shilingi Bilioni 1.3, Ujenzi wa bwawa Maratani Shilingi Milioni 450 na Fedha za kuchimbia visima virefu Milioni 50. Aidha, Serikali ipo mbioni kutekeleza Mradi Mkubwa wa Maji toka mto Ruvuma na kusambaza wilayani humo.

Katika ziara ya Waziri wa Afya aliyoifanya Nanyumbu, Mhe. Mbunge aliomba mashine ya Mionzi kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya na akapewa mashine yenye thamani ya zaidi ya Milioni 200. Tayari ujenzi wa jengo la Mionzi umekamilika. Aidha, Wizara pia imeipatia Nanyumbu Shilingi Milioni 400 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Afya Mtambaswa, Milioni 400 kwa ajili ya Ujenzi wa Wodi ya wazazi Mangaka na Milioni 200 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Afya Mikangaula.

Mheshimiwa Dua katika kutatua changamoto ya Mawasiliano wilayani Nanyumbu alifanikiwa kuwasilisha kero hiyo kwenye Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na tayari Nanyumbu imejengewa minara katika vijiji vya Magomeni, Sengenya, Songambele, Nangomba, Lowasa, Mkonona, Marumba, Chigweje, Chipuputa, Mkohora, Masuguru, Mtambaswala, Kazamoyo, Michiga, Nandete, Mnanje na Mkuula. Aidha huko Mbangala Mbuyuni na Napacho ujenzi wa minara unaendelea. Mhe. Dua pia ni Mjumbe katika Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Raphael Masimbo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Hamis H. Dambaya wamempongeza Mhe. Dua kwa namna anavyoshirikia vema na Halmashauri hiyo katika kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo

Mwenyekiti wa CCM Wilaya akifunga mkutano huo amewataka wajumbe pamoja na Watendaji wa Serikali katika ngazi ya Wilaya kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa moyo. Naye Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Didas Zimbihile amesisitia umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama.

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.