• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Majeshi ya Akiba kusimamia ujenzi wa Shule Chikotwa - Nanyumbu

Posted on: March 14th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Machali akimkabidhi Mifuko ya unga Mshauri wa Majeshi ya Akiba Nanyumbu Afande Kambanga ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kijiji cha Chikotwa


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Moses J. Machali amepokea mifuko kumi na mbili (12) ya unga kutoka kwa Ndg. Hamza Athumani Mkata (Meneja Kenoshukuru) ambaye ni mdau  wa maendeleo Nanyumbu na kumkabidhi Mshauri wa Majeshi ya Akiba Afande Kambanga ikiwa ni maandalizi ya majeshi hayo kwenda Kijiji cha Chikotwa Kushirikiana na wananchi katika ujenzi ya nyumba za walimu na madarasa.

Shule ya Msingi Chikotwa ilianza kama shule shikizi (Satelite school) ambayo ni tawi la Shule ya Msingi Nanyumbu I na kuwalazimu wanafunzi wakifika darasa la tatu (3) kuhamia Nanyumbu I. Aidha, umbali wa Kutoka Chikotwa kwenda Nanyumbu I ni takribani kilomita saba (7). Umbali huu uliwafanya wanafunzi wengi kuacha shule na kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi wasiohitimu darasa la saba. Pamoja na umbali huo pia mazingira hayakuwa rafiki kwa watoto kutembea katikati ya misitu ambayo kwa namna  moja au nyingine ilitishia usalama wao na hivyo kuilazimu Serikali Kuisajili Shule hiyo mwaka 2014. 

Shule ya Msingi Chikotwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa madarasa pamoja na nyumba za walimu jambo linalopelekea wanafunzi wa madarasa matano kurundikana darasa moja wakiwa na mwalimu mmoja tu shule nzima.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akizungumza na Ofisi ya Habari Nanyumbu amesema kuwa wananchi wakishirikiana na Majeshi ya Akiba wataanza ujenzi wa nyumba za walimu siku ya jumatatu  ya Tarehe 18/03/2019 asubuhi. Kutokana na zoezi hili Mhe. Machali amewaomba wadau mbalimbali wa Elimu kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule ili kuwawezesha walimu kupata sehemu ya kukaa ikiwa ni pamoja na kupata madarasa ya wanafunzi. Mkuu wa Wilaya amepokea kwa shukrani mchango wa chakula uliotolewa na Meneja wa Kenoshukuru na amewaomba wadau wengine kuichangia Chikotwa kwani bado inahitajika mifuko 100 ya saruji, bati, misumali, makopo ya rangi, nondo, mbao pamoja na mahitaji mengine ya ujenzi.

Ofisi ya Habari Nanyumbu imezungumza na baadhi ya wadau wa Elimu ambao wametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Wilaya na Majeshi ya Akiba kwa kushirikiana na wananchi wa Chikotwa kufanikisha Ujenzi wa miundombinu ya Shule. Aidha, wadau hao wamesema kuwa Mkuu wa Wilaya ametekeleza ndoto za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr, John Pombe Magufuli za kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya Elimu. Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa amekuwa akipeleka fedha kila mwezi katika shule zote za Msingi na Sekondari ili kuhakikisha hakuna mtoto yeyote atakayekosa Elimu kwa kukosa ada.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.