• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Maeneo ya utalii Nanyumbu yamvutia Naibu Waziri Maliasili na Utalii

Posted on: July 31st, 2018

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh.Japhet Hasungu (wanne toka kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo ya askari wa wanyamapori wakati alipotembelea hifadhi ya Lukwika Lumesule iliyopo Wilayani Nanyumbu

Wilaya ya Nanyumbu ni miongoni mwa Wilaya chache nchini Tanzania zenye vivutio vingi vya utalii ikiwemo hifadhi kubwa za wanyamapori, milima mirefu na yenye mawe ya ajabu, maeneo ya kihistoria pamoja na mito mikubwa yenye madaraja ya kiutalii. Akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu, Mh Japhet Hasungu (Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii) amesema kuwa ameshangazwa na kuvutiwa na mawe ya ajabu yaliyopo kijiji cha Lumesule katika Wilaya ya Nayumbu, hifadhi nzuri na kubwa ya wanyamapori ya Lukwika Lumesule pamoja na daraja la Umoja la Mtambaswala ambalo ni kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi. Mh. Naibu Waziri amewaagiza viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu kuhakikisha wanautangaza mara moja utalii huu mkubwa ili wageni na watalii toka ndani na nje ya nchi waje kutembelea vivutio hivyo.

Tanzania hakika hii ndiyo Edeni inayotajwa katika vitabu vitakatifu! ameyasema haya Mh. Hasungu huku akitaja utajiri mkubwa uliopo Tanzania kama maziwa na mito mikubwa, milima mirefu mfano Kilimanjaro, mbuga kubwa za kuvutia zilizojaa wanyama wa kila aina, uoto wa asili na ardi yenye rutuba, maeneo ya kihistoria ikiwa ni pamoja na vivutio vingine vingi ambavyo havipo katika mataifa mengine. Aidha, Mh Naibu Waziri amesema kuwa muda umefika sasa kwa kila mwananchi kujivunia na kuutangaza utalii wa nchi yetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Hamis H. Dambaya amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu inaendelea na jitihada ya kuibua na kutangaza vyanzo mbalimbali vya utalii. Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Salum Palango amemshukuru sana Mh. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuitembelea Nanyumbu na kutoa maelekezo mbalimbali ya namna ya kuiboresha sekta ya maliasili na Utalii. Aidha, Ndugu Palango amemhakikishia Mh. Naibu Waziri kuwa vivutio vyote vya utalii na maeneo yote ya kihistoria yataendelea kutangazwa na kuhifadhiwa ili kuboresha utalii na kukuza kipato cha Wilaya ya Nanyumbu na Taifa kwa ujumla.

Nanyumbu inawakaribisha watu wote wa ndani na nje ya nchi yetu kuja kutembelea hifadhi ya Wanyamapori ya Lukwika Lumesule, Kutembelea daraja la Umoja Mtambaswala pamoja na kujionea mawe ya ajabu, milima na maeneo mbalimbali ya kihistoria.  





Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.