• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Madaktari Nanyumbu watowa semina juu ya Saratani ya mlango wa kizazi

Posted on: April 25th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mh. Selemani Mzee (katikati), Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dr. Furaha Mwakafwila (kulia) na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya  Nanyumbu Ndg. Marco Mapunda (kushoto) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi wa Wilaya ya Nanyumbu wakimsikiliza kwa makini Mratibu wa Chanjo Nanyumbu Dr. Haridi Sungura (aliyesimama) wakati akielezea Kansa ya mlango wa kizazi mapema leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Dr. Sungura akitowa mafunzo hayo amesema kuwa:,

Saratani ya mlango wa uzazi ni mabadiliko ya ukuaji wa seli za mlango wa kizazi. Mabadiliko haya husababisha misuli au viungo vingine mwilini kuathirika. Saratani iliyojipenyeza ndani maana yake imesambaa na kushambulia misuli na viungo vingine ndani ya mwili. Saratani hii inaweza kusambaa na kuweza kushambulia kibofu cha mkojo, uke na sehemu ya chini ya utumbo mkubwa na baadaye figo, ini na sehemu zingine.

Saratani ya mlango wa kizazi ina athari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote. Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi, na  wengi wao wako katika nchi zinazoendelea. Saratani ya mlango wa kizazi inashuka nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake. Nafasi ya kwanza inashikwa na saratani ya matiti.

Karibu saratani zote za mlango wa kizazi husababishwa na virusi vya Human Papilloma. Kuna aina zaidi ya 40 ya virusi vya Human Papilloma vinavyoweza kusababisha maambukizi kwenye njia za uzazi za wanawake na wanaume, mdomoni na kwenye koo. Miongoni mwa wanawake wanaoambukizwa virusi hivi, asilimia 10 ndio hupata dalili za awali za ugonjwa wa saratani na baadaye saratani yenyewe baada ya miaka 10 hadi 20.

Visababishi vya maambukizi ni;

  • Kuanza kujamiana katika umri mdogo
  • Kuwa na wapenzi wengi
  • Kuwa na ndoa za mitala
  • Kuzaa watoto wengi
  • Uvutaji sigara

Dalili za Saratani ya mlango wa kizazi ni;

  • Kutokwa damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana
  • Maumivu ya mgongo, miguu na au kiuno
  • Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula
  • Kutokwa uchafu uchafu kwenye uke wa majimaji, uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu
  • Kuvimba mguu mmoja

Dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na;

  • Kuishiwa damu
  • Figo kushindwa kufanya kazi
  • Kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi

Kinga ya Saratani ya Mlango wa Kizazi

  • Kinga ya awali ni pamoja na:
  • Kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV vaccine),
  • Kubadili tabia,
  • Kuepuka ngono katika umri mdogo,
  • Kuepuka uvutaji wa sigara,
  • Kuepuka kubeba mimba katika umri mdogo na kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.
  • Kinga kwenye hatua za mwanzo ni kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za mwanzo na kupata matibabu stahiki.

Mkuu wa Wilaya Mh. Selemani Mzee amewapongeza watendaji wa Afya na kuwataka kufikisha mafunzo haya kwa jamii yote ya Nanyumbu ili kukabiliana na Saratani ya mlango wa kizazi. Aidha, amewataka watendaji wote wa Serikali ngazi ya Wilaya kuendelea kusimamia na kuhakikisha wasichana wote wenye umri wa miaka kumi na nne (14) wanajitokeza kupewa chanjo ya saratani hii zoezi lililoanza tangu tarehe 23/04/2018 na litakamilika tarehe 29/04/2018 katika Wilaya ya Nanyumbu.

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.