• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Kamati ya Siasa Mkoa wa Mtwara yatua Nanyumbu

Posted on: June 23rd, 2018

Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Ndugu Yusuph S. Nannila (anayeongea) imefanya ziara mapema leo katika Wilaya ya Nanyumbu kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ikiwa ni katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015. Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ilitolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Agosti 2015 ikionesha Dira ya maendeleo ya Taifa. Aidha, Katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020) Chama cha Mapinduzi kikiwa madarakani kimezielekeza Serikali zake kuhakikisha zinapambana na changamoto zinazozitajwa katika Ilani ambazo ni pamoja na; kuondoa umaskini, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na hasa kwa vijana, kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

Kamati ya Siasa Mkoa imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Nanyumbu. Miradi hiyo ni pamoja na:-

  • Matengenezo ya kawaida ya Barabara za Mangaka mjini (Km 6), Mangaka-Nachingwea (Km 34), Michiga-Mburusa (Km 17.3), Holola-Mnanje (Km 6.8), Mikuva-Ngupe (Km 5.8), Mnanje-Nakole (km 13) na Nandete-Ulanga (Km 10.9). Gharama ya ujenzi wa barabara hizi ni Shilingi 81,593,017.50 na kazi ya matengenezo ya barabara hizo inaendelea. 
  • Ujenzi wa Madarasa manne, ofisi mbili za walimu na vyoo kumi na mbili katika Shule ya Msingi Nahawara.
  • Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Chipuputa
  • Ujenzi wa Kituo cha Afya Mikuva
  • Mradi wa maji safi Nandete
  • Kukagua na kuona shughuli za kikundi cha BODABODA cha KM cha Mjini Mangaka

Uongozi wa Chama cha Mapinduzi umetoa pongezi za dhati kwa Wilaya ya Nanyumbu kwa kuratibu na kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo. Mwenyekiti wa CCM amekipongeza kikundi cha vijana cha BODABODA cha KM kwa kulipa mkopo wao waliokopeshwa na Halmashauri kwa wakati. Aidha, ameiagiza Halmashauri kuhakikisha inatowa mikopo kwa vijana na wanawake kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoagiza. Chama cha Mapinduzi pia Kimetowa mchango wa mifuko ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mikuva na ujenzi wa Ofisi ya kijiji cha Nahawara. Kamati ya Siasa imemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg Lwoga Musijaki  kuhakikisha mkandarasi aliyepewa mradi wa maji Nandete anakabidhi mradi kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji safi kwa haraka.

Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu wakizungumza na Ofisi ya Habari Nanyumbu wamesema wanaupongeza sana uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara kwa kuhakikisha unatembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ili kuona namna watendaji wa Serikali wanavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015. Aidha, wananchi wameendelea kutowa shukrani zao za dhati kwa Serikali kwa kuhakikisha zao la korosho linakuwa na soko zuri. Kamati ya Siasa Mkoa imewaahidi wananchi kuwa ipo nao bega kwa bega ili kuhakikisha kero za wanchi zinatatuliwa kwa wakati.



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.