Afisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Mashaka Mfaule (kulia) akifuatilia shughuli za ujenzi wa mnada wa mifugo.
Na, Lunanilo L. Ngela
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu inatekeleza mradi wa Ujenzi wa Mnada wa Mifugo katika kijiji cha Nanyumbu wilayani humo. Mnada huo ambao ujenzi wake unaendelea, utatumika kwa ajili ya biashara ya mifugo mbalimbali ndani na nje ya Wilaya hiyo.
Afisa Mifugo wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Mashaka Mfaume amesema kuwa, Halmashauri imetenga eneo hilo lenye ukubwa wa ekari kumi kwa ajili ya mnada huo. Aidha, Afisa huyo amesema mnada huo utawawezesha wafugaji kupata soko la uhakika la mifugo yao.
Ujenzi wa mnada huo unafanywa katika kijiji cha Nanyumbu pembezoni mwa barabara ya lami inayotoka Jamhuri ya watu wa Msumbiji kwenda Mji wa Mangaka mpaka Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.