• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Wilaya ya Nanyumbu yaendelea kung’ara Matokeo ya Kidato cha Sita 2023

Posted on: July 14th, 2023

Na, Lunanilo Ngela

Shule ya Sekondari Mangaka imeendelea kung’ara katika Matokeo ya Kidato cha Sita kwenye Mtihani wa Taifa wa Mwaka 2023 ambapo wanafunzi wote wamefaulu kwa asilimia 100.

Akizungumza na Ofisi ya Habari Nanyumbu, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mangaka Ndg. Geofray Kiula ameeleza kuwa, Wanafunzi 70 wa michepuo ya CBG na HKL walifanya Mtihani wa Taifa ambapo wanafunzi 12 walipata Daraja la Kwanza, wakifuatiwa na wanafunzi 52 waliopata Daraja la Pili huku wanafunzi sita waliobaki wakipata Daraja la Tatu.

Katika matokeo hayo, mwanafunzi Fadhila Athuman Athuman mwenyeji wa Kijiji cha Mtokora Kata ya Mangaka aliyesoma Kidato cha kwanza mpaka cha sita katika Shule ya Sekondari Mangaka amepata Daraja la 1.7 na kuamsha ari ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza mpaka cha nne katika shule hiyo kujiamini na kujituma zaidi darasani.

Kwa Mwaka 2022, Jumla ya wanafunzi 20 kati ya 59 waliofanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita walipata Daraja la Kwanza, wanafunzi 35 wakipata Daraja la Pili wakifuatiwa na wanafunzi wanne tuu waliopata Daraja la Tatu.

Serikali ilianzisha Kidato cha Tano mwaka 2020 katika Shule ya Sekondari Mangaka ikiwa ni Shule Pekee ya Kidato cha Tano na Sita wilayani humo na kupokea wanafunzi wa kike katika michepuo ya CBG na HKL

Wanafunzi wa Kidato cha Sita Katika Shule ya Sekondari Mangaka wameahidi kuandika rekodi nzuri zaidi katika Mitihani yao ya Taifa ya Mwaka 2024.

Wazazi na Wadau mbalimbali wa Elimu wametoa pongezi kwa wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo kwa jitihada zao za dhati katika kuhakikisha wanafunzi wanafaulu na kuendelea na masomo katika Taasisi za Elimu ya Juu. Aidha, wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari katika Wilayani hiyo.

Katika Mwaka 2023 Serikali Kuu imeipatia Wilaya ya Nanyumbu Jumla ya Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya ya Kitaifa ya Wasichana itakayojengwa eneo la Naishero Mangaka ambayo itakuwa na wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.

Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Mangaka kwa Mwaka 2023 wakiendelea na masomo darasani.

Wanafunzi wa Kidato cha Sita wajipanga kuacha rekodi nzuri katika Matokeo yao ya Mwaka 2024

Masomo yakiendelea darasani kwa wanafunzi wa kidato cha sita 2023.

Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mangaka wakiwa katika picha ya pamoja

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.