• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Waziri Ummy Mwalimu ashusha neema Nanyumbu

Posted on: December 6th, 2018

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Mji wa Mangaka huku akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Machali (Kushoto)


Na, Lunanilo L. Ngela

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) amefanya ziara ya kikazi mapema leo Tarehe 06/Disemba/2018 katika Wilaya na Nanyumbu na kuzungumza na  wananchi katika mkutano uliofanyika viwanja vya Kata ya Mangaka. Katika Ziara hiyo, Mhe. Waziri amezungumza na uongozi wa Wilaya, vyama vya Msingi vya ushirika pamoja na wananchi wote huku akitoa maelekezo mbalimbali na msimamo Serikali.

Ziara ya Mheshimiwa Ummy Mwalimu imekuwa neema kubwa kwa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuipatia hospitali ya Mangaka mashine ya Mionzi (X-Ray) mpya ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 200 pamoja na kuahidi shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa maabara ya Hospitali ya Mangaka. Aidha, Mhe. Waziri ameahidi kutatua tatizo la ikama ya watumishi wa Idara ya Afya wilayani Nanyumbu kwani kuna uhaba wa watumishi hao kwa asilimia 67.

Wizara ya Afya imepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli katika kuboresha Huduma za Afya kwa wananchi wote kwa kuhakikisha dawa zote mhimu zinapatikana mpaka ngazi ya zahanati. Katika Wilaya ya Nanyumbu dawa mhimu zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 95 huku bajeti ya dawa ikipanda kutoka Milioni 76 hadi Milioni 311 mwaka huu.

Waziri wa Afya amewahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa BIMA ya Taifa (NHIF) uitwao Ushirika Afya. Mfuko wa Ushirika Afya ni fao lililoanzishwa maalumu kwa ajili ya wakulima. Lengo la Serikali ni kuhakikisha inarahisisha matibabu kwa wananchi wote wakiwemo wakulima na sekta zisizo rasmi ili kuwawezesha kutibiwa katika vituo zaidi ya 6,500 nchini kote zikiwemo hospitali kubwa mfano Muhimbili. Katika Mfuko huu mwananchi atachangia Shilingi 76,800/= na kupatiwa kadi yake ya BIMA. Pamoja na faida mbalimbali za mfuko huu, watoto hawakuachwa nyuma kwani lipo fao maalumu kwa watoto ambalo mwanachama atachangia Shilingi 50,400/= na kumwezesha mtoto kutibiwa mahali popote nchini Tanzania.

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Nkurua akimshukuru Waziri wa Afya kwa kukubali ombi lake la kupatiwa mashine ya Mionzi kwa hospitali ya Mangaka, amesema kuwa mashine hii ni ukombozi mkubwa kwa wagonjwa wengi wa Wilaya ya Nanyumbu ambao hulazimika kusafiri mpaka Wilaya ya Masasi ili kupata huduma.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hamis H. Dambaya wametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Afya kwa kuimarisha huduma za afya. Aidha, wameahidi kuharakisha ujenzi wa jengo la Mionzi (X-Ray room) pamoja na maabara ya hospitali ya Mangaka ili kuboresha miundombinu ya hospitali na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za Afya wilayani Nanyumbu.

Ofisi ya Habari Nanyumbu imezungumza na wananchi mbalimbali ambao pamoja na Shukrani zao za pekee kwa Serikali ya awamu ya tano pia wameahidi kujiunga na mfuko mpya wa Ushirika Afya ili kujihakikishia matibabu bora. Aidha, wameiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama ili kulinda afya za wananchi.



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.