• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Wazazi Nanyumbu Wasaini Mkataba wa Uwajibikaji Mbele ya DC Magala

Posted on: September 7th, 2024

Na, Lunanilo Ngela

Wazazi na walezi wa wanafunzi wa darasa la saba katika shule za msingi zilizopo kata ya Masuguru, wilaya ya Nanyumbu, wamesaini mikataba maalum ya uwajibikaji iliyotayarishwa na wilaya hiyo. Lengo kuu la mikataba hiyo ni kuhakikisha kuwa wazazi wanatimiza wajibu wao kwa wanafunzi ambao wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mnamo Septemba 11-12, 2024.

Mikataba hiyo, iliyosainiwa tarehe 6 Septemba 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtambaswala, inamtaka kila mzazi au mlezi kumpatia mwanafunzi mahitaji yote muhimu yatakayomsaidia kufanya mtihani huo kwa ufanisi. Pia, wazazi wanawajibika kuhakikisha kuwa watoto wao wanahudhuria mitihani yote bila kukosa na kuchangia chakula cha wanafunzi wakati wa kipindi cha mitihani.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mheshimiwa Christopher Magala, alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mikataba hiyo, alibainisha kuwa hatua hii ni sehemu ya mikakati ya wilaya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata mazingira rafiki na salama ya kufanya mitihani yao kwa ufanisi. Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa wazazi kuwasimamia kikamilifu watoto hao ili waweze kutimiza ndoto zao.

Aidha, Mheshimiwa Magala alitoa onyo kali kwa wazazi ambao wanaripotiwa kuwa na tabia ya kuwashawishi watoto wao kufeli kwa makusudi katika mitihani. Alieleza kusikitishwa kwake na tabia hiyo, iliyobainika katika baadhi ya maeneo ya wilaya. "Ni jambo la kushangaza na kuhuzunisha kuona mzazi anamshawishi mtoto kuandika majibu ya uongo ili afeli katika mtihani wake," alisema Mkuu wa Wilaya huku akiwakumbusha wazazi kuwa elimu ya msingi na sekondari hutolewa bure kabisa nchini Tanzania.

Vilevile, Mheshimiwa Magala alimshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha kila shule inapokea ruzuku kila mwezi ili kugharamia shughuli zote za ufundishaji na ujifunzaji.

Kwa upande wake, Afisa Tarafa ya Nanyumbu, Ndg. Livinus Mchimbi, aliwasihi wazazi kutambua umuhimu wa elimu na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa watoto. Aliwakumbusha kuwa katika msimu wa kilimo wa 2024/2025, wakulima wa wilaya hiyo walilipwa kiasi cha shilingi bilioni 38.8 kutokana na uzalishaji wa zao la ufuta, ambapo kata ya Masuguru iliongoza kwa uzalishaji katika wilaya hiyo.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.