• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Wanaoirudisha nyuma Nanyumbu watauona moto asema DC Machali

Posted on: August 21st, 2018


Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali akitoa maelekezo kwa wakuu wa Taasisi za Umma pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali amefanya mazungumzo na Baraza la Madiwani Nanyumbu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za umma, pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Nayumbu. Katika mazungumzo hayo, Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi wote ikiwa ni pamoja na vipaombele vya Wilaya kwa sasa. Mhe. Machali amevitaja vipaombele vitatu kuwa ni Maji, Afya na Elimu ambavyo ni lazima kwa namna yeyote vipewe uzito wa juu katika kipindi cha uongozi wake.

Huduma ya maji kwa wananchi bado ni hafifu. Mhe Mkuu wa Wilaya amempa siku nne mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Nanyumbu kuhakikisha anampelekea mikakati ambayo Ofisi yake imeweka katika kutatua tatizo la maji kwa wakati. Aidha, Mkuu wa Wilaya ameshangazwa na kasi ndogo ya uchimbaji wa visima kwa kutumia mtambo wa Halmashauri na amewaagiza watendaji wa Idara ya maji kuhakikisha wanaongeza kasi ya uchimbaji wa visima. Mkuu wa Wilaya pia ameagiza kasi iongezwe katika utekelezaji wa miradi ya Mabwawa yatakayosambaza maji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa kupata fedha Shilingi Bilioni 140 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kuyatowa maji Mto Ruvuma na kuyasambaza katika vijiji.

Ujenzi wa zahanati vijijini, vituo vya afya na uboreshaji wa Hospitali ya Mangaka ni miongoni mwa maelekezo aliyoyasisitiza Mhe. Machali. Aidha, ameagiza kuwa kasi iongezeke katika ujenzi wa miuondombinu ya Afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya tangu ngazi ya kijiji, kata na hata Wilaya. Ujenzi huo ameagiza uende sambamba na ujenzi wa shule za msingi na Sekondari katika maeneo yasiyokuwa na shule. Wilaya ya Nanyumbu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018 imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya shule.

Mkuu wa Wilaya akizungumzia kilimo cha korosho ametowa onyo kwa viongozi wasio waadilifu wa vyama vya msingi wanaojinufaisha kwa kuiba fedha za wakulima kuwa Wilaya haitawaacha salama. Aidha, amekemea biashara haramu inayojulukana kama "kula maua". Hii ni biashara ambayo wafanyabiashara huwarubuni wananchi kwa kuwapa fedha au vitu na kuwataka walipe korosho ufikapo msimu wa mavuno. Mtu yeyote atakaye kamatwa akifanya biashara hiyo sheria itachukuwa mkondo wake.

Baraza la Madiwani limemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Joseph Magufuli kwa kumteuwa Mhe. Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nayumbu kwani anaendana na kasi walioihitaji kwa mda mrefu. Aidha, waheshimiwa Madiwani wamemwomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anawashughulikia kikamilifu wale wote ambao kwa maksudi wanarudisha nyuma maendeleo ya Nanyumbu. Nanyumbu inahitaji maji ya kutosha, Elimu bora na Afya wanasema waheshimiwa madiwani huku wakionesha msisitizo kwa Mkuu mpya wa Wilaya .







Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.