• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Wananchi Wilaya ya Nanyumbu wamshukuru Rais Magufuli kwa kununua korosho

Posted on: November 14th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Machali akipokea salamu za pongezi toka kwa  wakulima wa korosho wilayani Nanyumbu kwenda kwa Rais Magufuli leo Tarehe 14/11/2018


Na, Lunanilo Lunodzo Ngela

Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wa kununua korosho zote za wakulima kwa bei ya shilingi 3,300 umepokelewa kwa shamra shamra, vifijo na nderemo wilayani Nanyumbu. Katika hali ya kustaajabisha mapema Leo katika viwanja vya CCM wilayani Nanyumbu wamekusanyika wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi, vyama vya upinzani pamoja na wananchi wasiokuwa na itikadi za vyama wakiongozana na viongozi wa dini pamoja na viongozi wa jadi (Mamwenye na maapuya mwenye) ili kutoa shukrani zao za Pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli na wasaidizi wake kwa kuwasimamia wakulima wanyonge dhidi ya wafanyabiashara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa dini pamoja na wa jadi wamesema kuwa korosho kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ilipanda bei baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani hii ni katika Msimu wa kilimo 2015/2016 na imeendelea kuwa na thamani mpaka sasa. Viongozi hao wamesema walikata tamaa sana na kuumizwa mno na bei ndogo walizokuja nazo wanununuzi wa korosho katika msimu huu kwani zililenga kuishusha thamani korosho na kuwapoteza kabisa wakulima katika soko.

Waumini wa dini ya Kiislamu katika Wilaya ya Nanyumbu wamesema watakuwa na ibada maalumu ya kumwombea Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania siku ya tarehe 20/11/2018 katika kijiji cha Nahawara wilayani Nanyumbu ili aendelee kulitumikia vema Taifa na kuwakomboa maskini na wanyonge dhidi ya watu wasioitakia mema nchi yetu. Kwa upande wa waumini wa dini ya kikristo wakiwakilishwa na Padre wa kanisa la Romani Mangaka wameelezea furaha kubwa waliyonayo na wamemwomba Mheshimiwa Rais Magufuli kuendelea kuwapigania walipa kodi wa nchi hii na kutokatishwa tamaa na watu wachache wasioitakia mema Tanzania. Aidha, viongozi wa jadi  nao wakiwakilishwa na Katibu wa mamwenye (machifu) wa Wilaya ya Nanyumbu mwenye Hokororo (Matola) wamesema wana imani kubwa na Rais Magufuli na wamemwomba Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu kupeleka shukrani zao za pekee kwa Mheshimiwa Rais pamoja na wasaidizi wake.

Korosho ni zao kuu la biashara wilayani Nanyumbu na katika Mkoa wote wa Mtwara. Historia inaonesha kuwa zao hili lilimnufaisha mkulima wakati vilipokuwepo viwanda kabla ya watu wasiolitakia mema Taifa kuvichukua viwanda hivyo na kuvitokomezea mbali ili kuwanufaisha wafanyabiashara kwa miaka mingi kwa vile mkulima hakuwa na sehemu ya kupeleka korosho zake. Wakulima wanasimulia machungu waliyoyapitia katika kipindi kirefu kuwa korosho iliuzwa mpaka shilingi 100 kwa kilo mfano mwaka 2002. Aidha, wakulima wa korosho waliendelea kunyonywa na wafanyabiashara siku zote huku wakilipwa fedha chini ya shilingi 1,000 kwa kilo kwa kipindi kirefu na wakati mwingine kuambulia kukopwa korosho bila kulipwa chochote.

Historia hii ya maombolezo na vilio vya wakulima wa korosho ilibadilika katika kipindi cha uongozi wa Rais John Pombe Magufuli baada ya wanachi kukutana na bei za korosho ambazo hawakuwahi hata kuota kwani bei ilipanda kutoka shilingi 1,000 mpaka 4,500 kwa kilo. Ni katika kipindi hiki sasa maisha ya wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu yalibadilika na watu kupiga hatua kubwa kimaendeleo huku wakiutokomeza umaskini kwa nguvu. Nanyumbu wana kila sababu ya kuufurahia uongozi wa Rais Magufuli kwa vile umebadilisha kabisa historia ya kule walikotoka. Wananchi wa Nanyumbu wanasema kuwa walishangazwa sana na taarifa ya watu walioweka mawe na mchanga katika korosho zilizopelekwa nje ya nchi mwaka jana na wanaamini watu hao walilenga kuhakikisha wakulima wa korosho wanakosa soko. Aidha, wanasema kulikuwa na kila dalili za watu waovu kuingilia soko la korosho mwaka huu na kutafuta njia ya kuishusha bei na ikibidi kupoteza kabisa thamani ya korosho ili waendelee kujinufaisha huku mkulima akinyonywa jambo ambalo wakulima hawakuwa tayari.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Machali amefika eneo hilo la tukio na kupokea salamu zote za shukrani toka kwa wananchi na ameahidi kuzipeleka kwa Rais Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mheshimiwa Machali amepongeza sana uamuzi wa wananchi hao wa kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli. Aidha, Mkuu wa Wilaya ameahidi kusimamia kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Rais ya kuhakikisha kila mkulima analipwa stahiki yake. Mkuu wa Wilaya pia amepokea salamu za wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa Rais Magufuli zilizowasilishwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Paul Mwita.

Nanyumbu inajivunia uwepo wa Rais John Pombe Magufuli. Aidha, ni Wilaya pekee ambayo ilimpa kura nyingi zaidi katika Mkoa wa Mtwara.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mungu ibariki Wilaya ya Nanyumbu  


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.