• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Wakuu wa Wilaya Mtwara wasaini Mkataba wa Afua za Lishe

Posted on: September 10th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe, Gelasius Gaspar Byakanwa (Katikati) akizungumza jambo na Katibu Tawala Mkoa Dr, Jilly Elibariki Maleko (Kushoto kwake) wakati Wakuu wa Wilaya wakisaini Mkataba wa Afua za Lishe.  Waliokaa (Wa kwanza kulia)  ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa ameongoza kikao cha Tathmini ya lishe mkoani Mtwara kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya kujadili kwa kina hali ya utekelezaji wa Afua za lishe kwa mwaka 2017/2018, Mikakati ya namna ya kuboresha Lishe kwa kipindi cha Septemba - Juni 2019 ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara kutia saini Mkataba wa utekelezaji wa Afua za Lishe.

Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa na wajumbe walibainisha changamoto mbalimbali zinazozorotesha lishe mkoani Mtwara kuwa ni pamoja na matumizi ya chumvi isiyo na madini ya joto, wanawake wajawazito kutohudhuria kliniki, utapiamlo, kula kupita kiasi, kutofanya mazoezi ya viungo, upungufu wa damu na wanawake kujifungulia nyumbani. Mkuu wa Mkoa amewagiza watendaji wote katika sekta ya Afya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kujenga jamii ya watu wenye afya njema inayoendana na kasi ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda. Amewaagiza pia Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu makubaliano ya mkataba waliosaini wa Utekelezaji wa Afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tathmini inafanyika mara kwa mara ili kupima kiwango cha utekelezaji ambacho Wilaya imefikia.

Ofisi ya Habari Nanyumbu ilipata nafasi ya kuongea na Mhe. Moses Joseph Machali Mkuu Mpya wa Wilaya ya Nanyumbu ambaye alipongeza uamuzi wa Mkoa katika kusimamia Lishe na aliahidi kutekeleza kikamilifu makubaliano yote ya Mkataba wa Afua za Lishe. Mheshimiwa Machali amekuwa akisisitiza wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu kushiriki katika mazoezi ya viungo ili kujenga Afya bora inayoendana na kasi ya ujenzi wa Nanyumbu mpya. Aidha, wajumbe wa kikao waliiomba Wilaya ya Nanyumbu kutoa uzoefu wa namna ilivyofanikiwa katika kuhamasisha jamii kutumia huduma za Afya jambo lililopongezwa sana na uongozi wa Mkoa pamoja na washiriki wengine wa kikao.


"Lishe bora, kwa maendeleo ya Mtwara"




Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.