• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Ubalozi wa Msumbiji waitembelea Nanyumbu

Posted on: March 13th, 2019

Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe. Monica Patricio Kelement Musa (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Maratani na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali


Na, Lunanilo L. Ngela

Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe. Monica Patricio Kelement Musa ameitembelea Nanyumbu mapema leo na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J Machali. Katika ziara hiyo, Balozi ameongozana na maafisa kadhaa kutoka Ubalozi wa Msumbiji nchini Tanzania.

Mheshimiwa Monica Patricio Musa amesema kuwa Msumbiji inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Tanzania katika kupigania Uhuru wa nchi yao. Aidha, amesema kuwa Tanzania itaendelea kukumbukwa na mataifa mbalimbali ya ndani na nje ya Afrika kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia ukombozi  wa Bara la Afrika. Amesema pia kuwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere hakuwa tayari kuona nchi yake ikiwa huru huku mataifa mengine ya kiafrika yakiwa utumwani.

Ubalozi wa Msumbiji umetembelea kijiji cha Maratani ambako wapo raia wa Msumbiji waishio humo na kutoa bati sitini (60) na mifuko kumi na tano (15) ya saruji kwa shule mpya ya Sekondari Maratani ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha watoto wote  wanapata Elimu. Shule mpya ya Sekondari Maratani inategemea kufunguliwa wakati wowote tangu sasa baada ya kukamilika kwa baadhi ya miundombinu mhimu ya shule.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali amewakaribisha wananchi wa Jamhuri ya Msumbiji kuja kuwekeza Nanyumbu katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo viwanda. Mhe. Machali amesisitiza kuendelea kudumishwa kwa amani na mshikamano ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kisheria wakati wa kuvuka mpaka toka Tanzania kwenda Msumbiji au Msumbiji kuja Tanzania. Aidha, Mhe. Machali ametoa shukrani za pekee kwa Ubalozi wa Msumbiji kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwa Shule ya Sekondari Maratani.

Ofisi ya Habari Nanyumbu imezungumza na Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Salum A. Palango ambaye pamoja na kuushukukuru Ubalozi wa Msumbiji amesema muda umefika sasa kwa mataifa ya kiafrika kuacha mapambano ya bunduki na kuanza mapambano ya kiuchumi ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi. Nanyumbu imeendelea kuwa jirani mwema wa Msumbiji ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya.



Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Mradi wa Maji Mto Ruvuma, DC Magala Atoa Maagizo Mazito

    July 11, 2025
  • Nanyumbu Yatikisa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025

    July 10, 2025
  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.