Na, Lunanilo L. Ngela
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, wamewateuwa wagombea 42 wa udiwani katika Kata 17 za Jimbo la Nanyumbu watakaogombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Jumla ya wagombea 45 walichukua fomu wakiwepo wagombea 9 kutoka CUF, 17 CHADEMA, CCM wagombea 17 na wawili ACT Wazalendo.
Wagombea wafuatao wameteuliwa; Kata ya Mangaka ni Halima Mchoma (CCM) na Omari Maluchila (ACT Wazalendo). Kata ya Kilimanihewa Dadi Twenyuka (CHADEMA), Thabiti Geugeu (CCM) na Rehema Mwatuka (CUF). Kata ya Sengenya Mrera Adam (CHADEMA), Daimu Milanzi (CUF) na Msafiri Kasembe (CCM). Kata ya Likokona Hassan Likonda (CHADEMA) na Joseph Omari (CCM). Kata ya Michiga Ahamadi Malola (CHADEMA), Hashimu Nasiri (CCM), Adinani Mtila (ACT Wazalendo) na Moradi Moradi (CUF).
Kata ya Lumesule Mohamed Mlunji (CHADEMA), Salum Chuma (CCM) na Ally Nandonde (CUF). Kata ya Napacho Hamis Mnumbe (CHADEMA) na Matindiko Matindiko (CCM). Kata ya Chipuputa Bushiri Nyasa (CHADEMA) na Arabi Rabana (CCM). Kata ya Nanyumbu Hamis Nguku (CHADEMA), Husein Lasi (CCM) na Juma Kambutu (CUF). Kata ya Masuguru Benjamin Masimbo (CCM) na Namatolo Hassan (CUF). Kata ya Mkonona Mbelenje Shaibu (CHADEMA), Msafiri Njaidi (CUF) na Katoto Nyaraka (CCM).
Kata ya Maratani Mohamed Bakari (CHADEMA) na Salum Mmole (CCM). Kata ya Mnanje Athumani A. Chilala (CCM) na Mohammed Daraja (CUF). Kata ya Nandete Habil Kaine (CHADEMA) na Yustus Mmuni (CCM). Kata ya Mikangaula Zena Msanga (CHADEMA), Abdul Chiwila CCM na Shabani Mneke (CUF). Kata ya Kamundi Mlanzi Amandus (CHADEMA), Ali M. Ali (CUF) na Elevan Mussa (CCM) na Kata ya Nangomba Sijaona Makumbi (CCM).
Wagombea wasioteuliwa ni; Star Mamu wa (CHADEMA) Kata ya Mangaka (hajarudisha fomu), Kasimu Mpatia wa (CHADEMA) Kata ya Mnanje (hajarudisha fomu) na Athumani Mlaponi (CHADEMA) Kata ya Nangomba (hajarudisha fomu).
Aidha, Mgombea Sijaona Ajili Makumbi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Kata ya Nangomba amepita Bila kupingwa.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.