• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Nanyumbu yapongezwa kwa kupata Hati Safi Ripoti ya CAG

Posted on: June 14th, 2023

Katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

Na, Lunanilo Ngela

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kwa kupata Hati Safi (Unqualified Audit Opinion) katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo mapema leo Juni 14, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, wakati Baraza Maalum la Madiwani lilipoketi kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2022.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu isimamia kikamilifu ukusanyi wa mapato, usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuzuia hoja za ukaguzi, kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuhakikisha inaweka mfumo Madhubuti wa kusimamia mashine za ukusanyaji wa mapato (POS).

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi wa Divisheni ya Afya kujengewa uwezo wa namna ya kujaza vyema fomu za madai ikiwemo madai kwenda Bima ya Afya (NHIF) ili kuhakikisha fedha hizo zinalipwa kikamilifu kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.

Nae Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauter John Kanoni pamoja na kuipongeza Halmashauri kwa kupata hati Safi pia amesisitiza hoja zilizobaki kufungwa kabla ya Septemba 30, 2023.

Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hufanyika kila Mwaka baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 143(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, na Kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sura ya 418 na kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na Kamati za Kudumu za Bunge.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Masuguru Mhe. Benjamin Raphael Masimbo akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauter John Kanoni akizungumza na wajumbe wa Baraza Maalum la Madiwani


Katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Ibrahim John Mwanauta akizungumza katika mkutano wa Baraza Maalum la Madiwani

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Mtwara Bi. Janeth Kikoti akiwasilisha Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Baraza Maalum la Madiwani 

Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu CPA (T) Zauda F. Fundi akiwasilisha kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya kujadiliwa na wajumbe wa Baraza Maalum la Madiwani


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu wakiwa katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.