• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

Posted on: May 17th, 2025

Na, Lunanilo Ngela

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi, ameipongeza Wilaya ya Nanyumbu kwa kutekeleza miradi bora ya maendeleo inayozingatia falsafa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwahudumia wananchi.

Pongezi hizo zilitolewa Mei 17, 2025, wakati Mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa katika Wilaya ya Nanyumbu na kutembelea jumla ya miradi sita yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.27. Kati ya miradi hiyo, minne iliwekewa mawe ya msingi, huku miwili ikionwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Nachiura, Ndg. Ussi alisema:

"Ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwamba Halmashauri na Manispaa zetu zitenge fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Naipongeza Halmashauri ya Nanyumbu kwa kutekeleza maelekezo haya kwa vitendo."

Miradi mingine iliyowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Michiga, ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Namaguluvi, na ujenzi wa barabara ya Jarome pamoja na uendelezaji wa barabara ya Msangi kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita moja.

Vilevile, Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika shamba la miti la mfano lililoko Kijiji cha Chinyanyila pamoja na shughuli za kikundi cha madereva bodaboda cha Umoja ni Nguvu kilichopo Kijiji cha Mtokora.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala, alimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Abdallah Mwaipaya, baada ya kuwasili Mkoani humo ukitokea Mkoa wa Ruvuma. Katika Wilaya ya Nanyumbu, Mwenge huo umekimbizwa umbali wa kilomita 143.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 ni:

“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.”

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.