• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi aahidi neema shamba la mifugo Nangaramo

Posted on: March 31st, 2023

Katika picha ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (Mb) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariamu Chaurembo (kushoto) alipotembelea shamba la mifugo Nangaramo

Na, Lunanilo Ngela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (Mb) ametembelea shamba la mifugo Nangaramo wilayani Nayumbu Machi 31, 2023 na kuzungumza na wananchi waliojitokeza shambani hapo kumpokea ikiwa ni pamoja na kutembelea mabanda ya mifugo na kupokea taarifa ya uendeshaji wa shamba hilo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda ya mifugo shambani hapo, Mhe. Silinde amesema kuwa, Wizara inafanya jitihada kubwa ya kuboresha mifugo na kufanya uzalishaji uwe bora zaidi na wenye tija ili kuinua kipato cha wafugaji.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa, nia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan ni kufufua na kubadilisha maisha ya watanzania kupitia mifugo na uvuvi jambo ambalo Wizara hiyo imejipanga kutekeleza kwa vitendo.

Aidha, Mhe. Silinde ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali za shamba hilo ikiwemo upatikanaji wa maji, uhaba wa watumishi wa sekta ya mifugo wilayani Nanyumbu, uhaba wa miundombinu ya kunyweshea na kuogeshea mifugo pamoja na kutimiza ahadi zote zilizoahidiwa na viongozi wa Wizara hiyo katika kuboresha na kuongeza uzalishaji katika shamba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Khatibu Chaurembo akizungumzia changamoto katika Sekta ya Mifugo wilayani hapo amesema kuwa, Wilaya ina maafisa mifugo watatu tuu na hivyo kuiomba Wizara kuongeza watumishi ili kuharakisha maendeleo  wilayani hapo. Aidha, Mhe. Chaurembo ameongeza kuwa pamoja na Wilaya kufanya jitihada kubwa ya kupima na kutenga vitalu 100 vya wafugaji lakini bado kuna uhaba mkubwa wa miundombinu ya maji na majosho.

Kaimu Meneja wa Shamba Ndg. Wilbard S. Deograsias amesema kuwa, shamba la mifugo la Nangaramo lina ukubwa wa ekari 5,633.7 na lilianzisha mwaka 1970 kwa lengo la kuzalisha na kusambaza mitamba chotara ya ng’ombe wa maziwa kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.  Aidha, meneja huyo amemweleza Naibu Waziri kuwa shamba lina uwezo wa kubeba ng’ombe 2,700 ingawa kwa sasa lina ng’ombe 402 na hivyo kuiomba Wizara kuongeza mifugo hususani ng’ombe dume.

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.