• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mwenyekiti wa UWT Taifa aacha tabasamu Nanyumbu

Posted on: July 23rd, 2023

Katika picha ni Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda (wa pili kulia) akikagua ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Nanyumbu, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Chaurembo

Na, Lunanilo Ngela

Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu wamempokea kwa shamrashamra Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda, wakati alipotembelea Wilaya hiyo Julai 23, 2023 kwa ziara ya siku moja kukagua utekelezaji wa Ilani pamoja na kuzungumza na wananchi

“Nimewapenda bure” Alisema Ndg. Chatanda akifurahia umati wa wananchi wa Nanyumbu waliofurika kumpokea katika vijiji na vitongoji mbalimbali alivyotembelea kuona na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa UWT Taifa aliongozana na Ndg. Zainab Khamis Shomari Makamu Mwenyekiti UWT (Zanzibar), Dr. Phillis Nyimbi Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Ndg. Riziki Kingwande Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara, Ndg. Tunu Juma Kondo Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar pamoja na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa

Mwenyekiti wa UWT Taifa ametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Uongozi wa CCM Wilaya, Mbunge wa Jimbo, Watendaji wa Serikali, wanachama wa CCM pamoja na Wananchi kwa ujumla kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu, Afya, Barabara, Umeme na Maji

Akizungumzia mafanikio ya awamu ya sita katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo pamoja na Utoaji wa Huduma za Kijamii, Cde Chatanda amesema kuwa UWT ina Imani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba watamchukulia fomu ya kugombea Urais 2025 ili kukamilisha Miradi ya Kipaumbele na ya Kimkakati anayoitekeleza

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Khatibu Chaurembo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Yahya Ally Mhata wametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya hiyo Mabilioni ya fedha za Miradi ikiwemo zaidi ya Bilioni 58 zinazotekeleza miradi ya maji

Mwenyekiti wa UWT Taifa akikagua shughuli za ugawaji wa pembejeo za Kilimo

Mwenyekiti wa UWT Taifa (Kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nanyumbu Cde. Rashid Ally Mrope pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Salome Luhingulanya

Kutoka Kushoto ni Mbunge wa Jimbo Mhe. Yahya Mhata, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Cde. Rashid Mrope, Mkuu wa Wilaya Mhe. Mariam Chaurembo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Benjamin Masimbo na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Ibrahim Mwanauta wakifurahia ziara ya Mwenyekiti UWT Taifa

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hadija Alphani Hamisi akizungumza katika mkutano Kijiji cha Mikangaula

Mwenyekiti wa UWT Taifa akisalimiana na Katibu wa UWT Wilaya ya Nanyumbu Cde. Halima Iddi Tina

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo Halmashauri



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.