Katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Marium Khatibu Chaurembo
Na, Lunanilo Ngela
Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu wameshauriwa kulima mazao ya chakula na biashara kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora ikiwemo matumizi ya mbegu bora, mbolea na viuatilifu vya kudhibiti magonjwa na wadudu wanaoharibu mazao.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Marium Chaurembo wakati akizungumza na Maafisa kilimo na watendaji ngazi ya kata na vijiji ikiwa ni sehemu ya mkakati maalum wa kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na ufugaji ili kuongeza pato la mwananchi.
Mkuu Wilaya amewaagiza maafisa kilimo na mifugo kutengeneza ratiba ya utoaji chanjo ya mifugo kama kuku ili kuepusha mifugo hiyo kufa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya ufugaji wa kisasa.
Wananchi wamesisitizwa kuandaa mashamba mapema kwa ajili ya kilimo, kupanda mbegu bora kwa kuzingatia mistari na nafasi sahihi, kufanya palizi na kuvuna kwa wakati. Aidha, Mhe. Chaurembo amewataka wananchi kulima pia mazao yanayohimili ukame au mvua kidogo ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.