• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aagiza walioiba fedha ya wakulima Nanyumbu kukamatwa

Posted on: April 10th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Gelasius Gasper Byakanwa ameipokea taarifa ya Tume ya uchunguzi iliyoteuliwa kwenda kujiridhisha kama wakulima wote wa Wilaya ya Nanyumbu wamelipwa fedha ya Korosho katika msimu wa kilimo 2017/2018. Tume ilikuwa na wajumbe watano ambao walitoka Ofisi tofauti ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, TAKUKURU, POLISI na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. Mwenyekiti wa Tume Ndg, Severine Msonda akisoma taarifa ya Tume mbele ya Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Wilaya ya Nanyumbu ina vyama 37 na vyote vimepitiwa na tume. Aidha, vyama vya msingi hivyo vilikusanya kilo 20,205,121 za korosho kwenye matawi na  kupeleka maghala makuu (ware house) kilo 19,757,495 na kulipwa Shilingi 72,986,102,050/=. Tume imebaini kuwa jumla ya kilo 225,296 za wakulima hazijalipwa mpaka sasa huku vyama vikiwa havina hela jambo lililosababishwa na ubadhilifu wa baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi ikiwa ni pamoja na uzembe. Aidha, Timu imetoa takwimu ya vyama vyote vilivyopoteza korosho, wahusika pamoja na kiasi cha fedha kinachotakiwa kurudishwa ili wakulima walipwe pesa zao.

Mkuu wa Mkoa amelaani vikali wizi uliofanywa na baadha ya viongozi wa vyama vya msingi  ikiwepo chama cha Napacho ambako yalifanyika malipo hewa ya Tshs Milioni 209,000,910/= ambazo waliingiziwa watu wasiouza hata punje ya kurosho. Mkuu wa Mkoa ameviagiza Vyombo vya vya Ulinzi na Usalama kuwakamata wale wote walioingiziwa malipo kwa kuuza korosho hewa, pamoja na wote ambao kwa namna moja au nyingine wametajwa na Tume kuwa wamefanya wizi/ubadhilifu.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mh. Selemani Mzee amesema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama inaanza leo kupokea malamiko ya wakulima kuhusiana na korosho katika ukumbi wa Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu wote waliohusika katika wizi huo. Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu wametowa shukrani zao za pekee kwa Mkuu wa Mkoa na Uongozi wa Wilaya kwa kuingilia kati mgogoro huu. Aidha, wameiomba Serikali kuendelea kuwa karibu na wakulima ikiwa ni pamoja na kuzileta pembejeo kwa wakati ili kufanikisha uzalishaji wa korosho katika msimu wa kilimo 2018/2019.




Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.