• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mbunge Nanyumbu aongoza harambee kuchangia Ujenzi wa shule

Posted on: December 20th, 2018

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Willium Nkurua (Kulia) akizungumza na wananchi katika harambee na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Emmanuel Kapinga


Na, Lunanilo L. Ngela

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Willium Nkurua ameongoza wananchi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari Masuguru ili kuiwezesha shule hiyo kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema 2019. Harambee hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Nanyumbu pamoja na wananchi wa Kata ya Masuguru.

Mheshimiwa Mbunge amewahamasisha wananchi na wadau mbalimbali katika kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ili kuhakikisha shule inakamilisha majengo yote mhimu na kuiwezesha kusajiliwa na Wizara ya Elimu. Katika Kata ya Masuguru wanafunzi husafiri zaidi ya Kilomita arobain (40) kwenda shule ya sekondari Nanyumbu ili kupata Elimu hali inayopelekea wanafunzi wengi kutohitimu kidato cha nne.

Katika Harambee hiyo, jumla ya mifuko 161 ya simenti (taslimu na ahadi) imechangwa ikiwa ni pamoja na ahadi ya shilingi 3,761,900/=  pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi 731,400/=  ili kuwezesha ujenzi huo. Aidha, wananchi wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha shule ya Sekondari Masuguru pamoja na Maratani zinakamilika na kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu. 

Diwani wa kata ya Masuguru  Mhe. Benjamini Masimbo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, ameiomba Serikali kukubali shule hiyo ya Masuguru kufunguliwa mapema mwakani ili kuwawezesha wanafunzi kusoma hapo huku wakiondokana na tatizo la kusafiri zaidi ya kilomita arobaini Mpaka kata ya Nanyumbu kufuata shule.

Wananchi wa Kata ya Masuguru wakizungumza na Ofisi ya Habari wametoa pongezi za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua W. Nkurua kwa namna anavyoshirikiana nao katika kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Nanyumbu. Mheshimiwa Dua (Mb) wiki mbili zilizopita alijenga hoja mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya kuomba kupewa mashine ya Mionzi kwa ajili ya Hospitali ya Mangaka, hoja iliyozaa matunda na Hospitali kupewa mashine mpya ya kisasa ya Mionzi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.




Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.