• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mbio za Mwenge wa Uhuru zakamilika rasmi wilayani Nanyumbu

Posted on: June 12th, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hamis H. Dambaya (kushoto) akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi Gimbana Ntavyo mapema leo katika Halmashauri ya Mji wa Masasi baada ya kukamilika kwa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Nanyumbu. Mkurugenzi huyo wa Nanyumbu akiwahutubia maelfu ya wananchi na viongozi waliofurika kwa ajili ya kuupokea Mwenge wa Uhuru, ametoa shukrani za pekee kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho na kusema kuwa akiwa katika wilaya ya Nanyumbu kiongozi huyo amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa fedha za Umma zinatumika vizuri.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Nanyumbu umekimbizwa umbali wa Km.186.8 zilizo ndani ya Tarafa tatu kati ya nne za Wilaya ya Nanyumbu ambazo ni Nakopi, Mangaka na Maratani.

Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Nanyumbu umepitia miradi Kumi na moja (11)  yenye thamani ya shilingi 1,449,089,543/= kutoka vyanzo vinne ambavyo ni:- (i) michango ya wananchi Shilingi 47,810,170 sawa na asilimia tatu, (ii) Halmashauri ya Wilaya shilingi 394,350,273/= sawa na asilimia ishirini na saba, (iii) Serikali Kuu Shilingi 209,129,100/= sawa na asilimia kumi na nne (iv) Wahisani shilingi 797,800,000/= sawa na asilimia hamsini na sita. Aidha, katika miradi hii Mwenge wa Uhuru umefungua miradi miwili, umeweka jiwe la msingi mradi mmoja, umekaguwa miradi minne na kuzinduwa miradi mitatu.

Kiongozi wa  mbio za Mwenge Kitaifa akiwaaga viongozi na wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu ameipongeza Wilaya ya Nanyumbu kwa mapokezi mazuri ya Mwenge pamoja na ukarimu wao mkubwa waliouonyesha kwa wakimbiza Mwenge. Aidha, ameipongeza Wilaya ya Nanyumbu kwa kuwa na miradi bora yenye tija kwa wananchi. Kiongozi wa mbio za Mwenge pia amepongeza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji yaliyopelekea Wilaya ya Nanyumbu kupiga hatua nzuri ya Kimaendeleo.

Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu wametoa pongezi zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli na kumshukuru kwa kuhakikisha bei ya korosho inakuwa nzuri. Aidha, wananchi wametoa shukrani zao za dhati kwa kupata bahati ya kutembelewa na Mwenge wa Uhuru. Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu walijaa barabarani na katika maeneo yote ambako Mwenge wa Uhuru umefika ili kuupokea.

Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 ni "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA; WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA".


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.