• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Makundi ya wafugaji yaliyoingia Nanyumbu bila vibali yapewa siku 5 kuondoka

Posted on: September 9th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Khatibu Chaurembo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lumesule

Na, Lunanilo Ngela

Wafugaji waliovamia mashamba ya wakulima Wilaya Nanyumbu wakitokea maeneo mbalimbali wamepewa siku tano kuanzia Septemba 9, 2023 mpaka Septemba 13, 2023 (Jumatano) kuhakikisha wanaondoka katika maeneo hayo.

Maelekeo hayo yametolewa mapema Septemba 9, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Chaurembo wakati akitatua kero za wananchi wa kijiji cha Lumesule ambao wamelalamikia kuharibiwa mazao yao na wafugaji hao

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya wanakijiji wamemweleza kuwa, wafugaji hao huchunga mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na pindi wanapojaribu kuwazuia huambulia kipigo ikiwa ni pamoja na kuharibiwa mali zao

Akizungumza katika Mkutano huo, Mkuu wa Wilaya amewaeleza wananchi hao namna Ofisi yake inavyolishughulikia swala hilo kwa ukaribu na kuwasihi wananchi hao kutojichukulia sheria mkononi

Aidha, Mhe. Chaurembo amesema kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ambako baadhi ya wafugaji hao hutoka huko na kuvuka mipaka ya Wilaya yao kufuata malisho ya mifugo  Nanyumbu na baadae kurudi kwao

Naye Afisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. mashaka Mfaume amemweleza Mkuu wa Wilaya kuwa, hakuna kibali chochote kilichotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu cha kupokea wafugaji katika eneo linalolalamikiwa na wananchi hao wa Lumesule na hivyo kuiomba serikali kuwaondoa wafugaji hao ili kurejesha utulivu wa vijiji hivyo

Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nanyumbu  Afande Severine Msonda akizungumza na wananchi wa Lumesule amewaeleza umuhimu wa kufuata sheria wakati wa kutatua migogoro ikiwa ni pamoja na kuwaonya wananchi hao kutojichukulia sheria mkononi



Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yajipanga Kukusanya Bil. 4.7 Mwaka 2025/2026 – DED Mwanauta Atoa Maelekezo Muhimu

    July 14, 2025
  • Mradi wa Maji Mto Ruvuma, DC Magala Atoa Maagizo Mazito

    July 11, 2025
  • Nanyumbu Yatikisa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025

    July 10, 2025
  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.