• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Maazimisho ya Kilele cha wiki ya Wazazi Nanyumbu yafanyika Mangaka Sekondari

Posted on: April 5th, 2018

.Mada mbalimbali zatolewa

.Shule ya Msingi Chikotwa ina mwalimu mmoja na wanakijiji hawataki walimu

.Utoro wa wanafunzi uliokithiri waidhoofisha Idara ya Elimu Sekondari

.Baraza la wazazi Nanyumbu latoka na maazimio ya moto

Maazimisho ya Wiki ya Wazazi kiwilaya yamefanyika leo Tarehe 05/04/2018 katika Shule ya Sekondari Mangaka huku wazazi wakitoka na maazimio mbalimbali ya kuinua taaluma ikiwa ni pamoja na kusimamia maadili. Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Mkoa wa Mtwara Ndg, Hussein Kasuguru ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi wa kilele hicho amewataka wazazi kusimamia maadili na kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unaongezeka ili kupata vijana bora wenye tija kwa Taifa. Ndg, Juma Muruwa ambae pia ni mjumbe wa Baraza kuu la wazazi Taifa ameipongeza Wilaya ya Nanyumbu kwa kuwa na ushirikiano mzuri baina ya watendaji wa Serikali na kufanya Ilani kutekelezeka

Katibu wa Wazazi Mkoa wa Mtwara Ndg, Mohamed Omari akizungumzia suala la mporomoko wa maadili amesema Jumuia ya Wazazi ina wajibu wa kusimamia malezi ya vijana na watoto. Aidha, amezitaja sababu mbalimbali za kuporomoka kwa maadili kuwa ni pamoja na Jamii kuacha mila na desturi, kutelekezwa kwa watoto na kuvunjika kwa ndoa. Katibu wa Wazazi Mkoa wa Mtwara ameitupia jicho Idara ya Elimu na kusema katika kuinua Elimu ni mhimu sasa wazazi wakifungua ukurasa mpya wa mahusiano mazuri na walimu ili kujua maendeleo ya watoto shuleni, kuhakikisha watoto hawapewi simu za mkononi wakiwa shule na kwamba ajenda ya malezi iwe ya kudumu. Ndg, Mohamed Omari amewakumbusha Maafisa Elimu kuhakikisha walimu wanafundisha mada zinazoendana na mihutasari ikiwa ni pamoja na kusimamia maadili ya walimu.

Kaimu Afisa Elimu Msingi Ndg, Noeli Chola aliliomba Baraza la Wazazi kufanya kazi kwa karibu na Idara ya Elimu kwani kuna baadhi ya vijiji wazazi hawatoi ushirikiano. Akitolea mfano wa Shule ya Msingi Chikotwa katika kata ya Nanyumbu ina mwalimu mmoja kwa mda mrefu na kila Idara inapotaka kupeleka walimu wanakijiji wamekuwa wakiweka vikwazo. Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ndg Seifu Zuberi amesema kuwa suala la Mdondoko wa wanafunzi katika shule za Sekondari wilayani Nanyumbu limekithiri na kufanya  wanafunzi wachache sana kuhitimu Elimu ya Sekondari. Angela Aore ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii amewataka wazazi kuwa wajasiliamali huku Asia Mkini Afisa ustawi wa jamii akikemea unyanyasaji wa watoto. Kitengo cha Utamaduni kikiwakilishwa na Zainabu Mgeni kimewataka watu kutetea utamaduni wa Taifa letu ikiwa ni pamoja na kuitaka jamii kuanzisha vikundi vya ngoma.

Katibu wa Wazazi wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Mshihiri pamoja na M/Kiti Wazazi wa Wilaya ya Nanyumbu wamewaagiza wazazi katika kila eneo kuhakikisha wanatekeleza maazimo yaliyofikiwa katika Baraza, aidha wamesema kuwa Jumuiya ya wazazi Wilaya haitasita kuchukua hatua mara moja kwa wale wote ambao hawatatekeleza majukumu yao. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni       "Sisi wazazi tupo imara kusimamia malezi na maadili ya watoto wetu".



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili June 11, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • RC Sawala Apongeza Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kilimanihewa, Awataka Wananchi Kuendeleza Ushirikiano

    June 11, 2025
  • DC Magala Afungua Mafunzo ya Jeshi la Akiba Nanyumbu

    June 10, 2025
  • "Tutachukua Hatua Kali kwa Watakaohujumu Wakulima" DC Magala

    June 09, 2025
  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.