• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Maajabu ya Pango la Habiba kuvuta watalii Nanyumbu

Posted on: October 16th, 2018

Katika picha hiyo ni barabara inayoingia wilayani Nanyumbu kutoka Mkoa wa Ruvuma


Na, Lunanilo L. Ngela

Nanyumbu ni miongoni mwa Wilaya chache sana nchini Tanzania zenye maeneo adimu ya kihistoria pamoja na vivutio vya kipekee vya utalii. Wilaya hii iliyopo mkoani Mtwara  ipo Kilomita 54 kutoka Masasi katika barabara ya Mtwara - Songea. Aidha, inapakana na Wilaya ya Nachingwea kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Masasi kwa upande wa Mashariki, Jamhuri ya watu wa Msumbiji kwa upande wa kusini na Wilaya ya Tunduru kwa upande wa Magharibi.

Pango la Habiba ni miongoni mwa vivutio vya kihistoria vilivyovuta hisia za watu wengi ndani na nje ya Wilaya ya Nanyumbu. Pango hili  lipo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Lukwika Lumesule. Ili kulitembelea pango hili ni vizuri ukifahamu baadhi ya Mambo ya kihistoria. Ikumbukwe kuwa Hifadhi hii ya wanyamapori (Lukwika Lumesule game reserve) inapakana na Kata ya Lumesule ambako ndiko lilikopiganwa pigano la mwisho la vita vya majimaji. Zipo baadhi ya kumbukumbu katika Mlima Makong'ondera ikiwepo mifupa ya kale pamoja na mafuvu katika mapango yanayosadikiwa kuwa huenda ni wapiganaji wa vita vya majimaji vilivyoongozwa na Kinjekitile Ngwale (1905-1907)

Hifadhi ya Lukwika Lumesule hutenganishwa na Mto Ruvuma ambao hugawa hifadhi hii upande wa Tanzania na Msumbiji. Serikali ya Tanzania kupitia mapato yake ya ndani ikishirikiana na Jamhuri ya watu wa Msumbiji ilifanikiwa kujenga Daraja la kisasa la Umoja huko Mtambaswala ambalo ni kivutio kikubwa cha Utalii katika Wilaya ya Nanyumbu. Ofisi ya Habari Nanyumbu wakati ikienda kulitembelea pango la Habiba  ilipata bahati ya kufika daraja la Mtambaswala na kupokelewa na Ndg. Salum Lihame Mwamba (Afisa mahusiano) na kubahatika kukutana na simulizi za Mtambaswala.

Salum Lihame Mwamba ambaye ni mtunza kumbukumbu za historia ya daraja la Umoja Mtambaswala anasimulia namna wajerumani walivyofika Mtambaswala wakati wa vita kuu ya kwanza ya Dunia (1914-1918) na namna vita ilivyopiganwa wakati wajerumani wakitafuta njia ya kuvuka kwenda Msumbiji wakitokea Tanganyika. Ukifika Mtambaswala utaoneshwa maeneo hayo ya kivita, lakini pia utafanikiwa kuifahamu vizuri historia ya Utumwa na namna soko la Mkunazini Zanzibar lilivyofungwa na baadhi ya raia walioachwa huru walivyofika Mtambaswala. Ukiwa Mtambaswala utafanikiwa pia Kuliona Daraja linalotembea pamoja na kuiona mbuga nzuri ya Lukwika Lumesule ambayo ndio Hifadhi pekee ambayo tembo mkubwa kuliko wote Afrika Mashariki na kati alipatikana humo.

Safari ya Kuelekea pango la Habiba huwafurahisha wengi kwani ukiwa njiani utapita kijiji cha Nakopi kwenye Mlima Majeja ambao juu yake kuna tumbaku ya ajabu na mtu yeyote anaruhusiwa kuvuta akiwa kule mlimani kwa masharti ya kutoondoka nayo kwani ukiondoka nayo lazima utapotea. Mlima huu hufanana sana na ule wa Chitowe ambao una pipa lisilofikika na pipa hili lilikuwepo tangu kipindi cha Ukoloni wa kijerumani.

Miongoni mwa vivutio vilivyopo Nanyumbu ni pamoja na Chemchem ya maji moto  katika Mto Ruvuma kitongoji cha Nangale kijiji cha Lukula. Maji haya ni ya moto yenye uwezo wa kuivisha hata mahindi. Aidha, ipo ardhi inayotikisika katika kijiji cha Namatumbusi. Pango la Habiba hili ni pango maarufu sana katika Hifadhi ya wanyamapori ya Lukwika Lumesule. Pango hili pamoja na mwonekano wake wa kipekee lakini pia huwa msaada mkubwa kwa binadamu na wanyama pindi wapatapo matatizo. Yupo Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Habiba alipata msaada wa pango hilo wakati akiwakimbia watu waovu na akatoka salama mikononi mwao. Hii ndio asili ya Jina Pango la Habiba.


Tukutane Nanyumbu, Kumenoga  



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.