• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

Posted on: July 3rd, 2025

Katika picha ni Shazimita Mohamed Adam akiwa katika moja ya karakana mjini Mangaka

Na; Lunanilo Ngela

Katika mji wa Mangaka, Wilaya ya Nanyumbu, msichana mdogo mwenye umri wa miaka 17 ameibua mshangao na kuvutia hisia za wengi baada ya kuonekana akifanya kazi ya uchomeleaji (welding), kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na wanaume pekee.

Huyu si mwingine bali Shazimita Mohamed Adam, mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari ya Naishero. Alianza kujifunza fani hiyo mwezi Novemba 2022, mara baada ya kumaliza darasa la saba, kwa nia ya kujipatia ujuzi utakaomsaidia kujiajiri na kujitegemea katika maisha yake ya baadaye.

"Niliamua kuchagua uchomeleaji kwa sababu siyo kazi inayofanywa na wasichana wengi. Nilijua itanipa nafasi ya kipekee katika soko la ajira na kunijengea heshima," anasema Shazimita kwa kujiamini, macho yake yaking’aa kwa matumaini.

Licha ya kuwa bado shuleni, Shazimita hutumia siku za Jumamosi na Jumapili kwenda kwenye karakana moja mjini Mangaka karibu na mgahawa wa mabatini kujifunza kwa vitendo. Anaifanya kazi hiyo kwa moyo wote, huku ndoto yake kubwa ikiwa ni kumiliki karakana ya kisasa na kutoa ajira kwa vijana wenzake.

Shazimita anaamini kuwa elimu ya ufundi ni mkombozi wa kiuchumi kwa vijana, na anaunga mkono wito wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, aliyewahimiza vijana kujiunga na vyuo vya ufundi kama VETA ili kujenga taifa lenye watu wenye ujuzi na uwezo wa kujitegemea.

"Ningependa shule za msingi na sekondari zianze kufundisha masomo ya ufundi. Tukianza mapema, tutajenga jamii yenye ujuzi na isiyopenda utegemezi," anasisitiza Shazimita.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia (2021), zaidi ya asilimia 60 ya vijana barani Afrika hukumbwa na changamoto ya ajira rasmi. Mataifa kama Ujerumani tayari yamepunguza tatizo hilo kupitia mfumo wa elimu ya ufundi wa vitendo (Dual Vocational Training System), ambapo zaidi ya nusu ya wanafunzi hujiunga na mafunzo hayo kuanzia ngazi ya chini.


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.