• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

FUM Nanyumbu Yavunja Rekodi ya Mapato na Kuandika Historia Mpya ya Miradi

Posted on: June 18th, 2025

Na, Lunanilo Ngela

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Benjamin Raphael Masimbo, amewapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya rasilimali za Halmashauri, akisema watakumbukwa daima kwa uzalendo na bidii yao ya kazi.

Akizungumza katika kikao cha mwisho cha kamati hiyo kilichofanyika Juni 18, 2025, katika ukumbi wa Halmashauri, Mhe. Masimbo alieleza kuwa wakati Kamati hiyo inaanza kazi mwaka wa fedha 2020/2021, Halmashauri ilikuwa inakusanya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 2.1. Hata hivyo, kutokana na usimamizi madhubuti wa kamati hiyo, “makusanyo hayo yameongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 4.2 katika mwaka wa fedha 2024/2025.”

Miongoni mwa mikakati iliyochangia mafanikio hayo ni pamoja na kudhibiti ununuzi holela wa mazao kama korosho, ufuta na mbaazi nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani; kuanzisha na kuimarisha vizuizi vya kudhibiti utoroshwaji wa mazao; kubuni vyanzo vipya vya mapato; na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa vyanzo vilivyopo ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi.

Katika kipindi hicho cha miaka mitano, miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 imetekelezwa Idara ya Elimu Msingi kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri, ruzuku kutoka Serikali Kuu, pamoja na michango ya wafadhili na wananchi. Miradi hiyo imejumuisha ujenzi wa vyumba 88 vya madarasa, ofisi 52 za walimu, nyumba 10 za walimu, na matundu 252 ya vyoo na madawati 1,320 yametengenezwa. Aidha, shule mbili mpya za msingi Kilimanihewa B na Napalavi zimejengwa.

Kwa upande wa elimu ya sekondari, miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 7.4 imetekelezwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya nne za sekondari (Mkapa, Naishero, Rukumbi na Kilimanihewa), ujenzi wa vyumba 108 vya madarasa, majengo manne ya utawala, ofisi 32 za walimu, nyumba 12 za walimu, matundu 128 ya vyoo, maabara 13, bwalo moja la chakula, mabweni 21, hosteli 2, vyumba vinne vya TEHAMA, maktaba 4. Vilevile, viti 2,711 na meza 2,805 zimetengenezwa.

Aidha, kwa upande wa sekta ya afya, miundombinu ya huduma za afya yenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 imetekelezwa. Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa jengo la dharura (EMD), jengo la mionzi, jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), maabara, bohari ya dawa na vifaa tiba, pamoja na ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Mangaka. Vilevile, vituo viwili vya afya vya Mnanje na Mikangaula vimejengwa, sambamba na ujenzi wa zahanati mpya 14

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg. Ibrahim John Mwanauta, ameipongeza Kamati hiyo kwa uadilifu, uwajibikaji na uzalendo wao katika kusimamia mapato na utekelezaji wa miradi. "Wajumbe wa Kamati hii wamekuwa mfano wa kuigwa. Mchango wao utabaki kuwa sehemu ya historia ya mafanikio ya Nanyumbu," alisema Ndg. Mwanauta.


Matangazo

  • Matokeo ya Usaili wa Kuandika wa Watunza Kumbukumbu Daraja la II June 28, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • FUM Nanyumbu Yavunja Rekodi ya Mapato na Kuandika Historia Mpya ya Miradi

    June 18, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.