• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Elimu ya Mpiga Kura

Posted on: March 6th, 2024

Elimu ya Mpiga Kura ni elimu ambayo hutolewa kwa wananchi wote kwa lengo la kuwawezesha kuelewa kuhusu Sheria, Kanuni, Taratibu za mchakato mzima wa Uchaguzi, wajibu wao na umuhimu wa kushiriki katika Uchaguzi, ni elimu isiyokuwa na hisia, ubaguzi wala itikadi za kisiasa.

Elimu ya Mpiga Kura inalenga kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakao waongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala Bora nchini.

Dhana hii ya Elimu ya Mpiga Kura inahusisha pia usambazaji wa taarifa, vielelezo na vipindi mbalimbali katika Vyombo vya Habari ambavyo vinalenga kuwaelimisha Wananchi juu ya mchakato wa Uchaguzi. Mchakato huu unahusisha Uandikishaji wa Wapiga Kura, Ugawaji wa Majimbo, Uwekaji wazi Daftari, Kampeni, utaratibu wa Kupiga Kura na vituo vya Kupiga Kura.

Elimu ya Mpiga Kura hutolewa kuhakikisha kuwa Wapiga Kura wanahamasika na wanakuwa tayari kwa hiyari yao, kwa ufahamu wao na kwa kujiamini kwao kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi wakiwa na mtizamo wa kukuza demokrasia.

Umuhimu wa Elimu ya Mpiga Kura

Elimu ya Mpiga Kura ni nyenzo na kielelezo muhimu katika kumuwezesha kila mwananchi kuelewa kuhusu mchakato wa Uchaguzi na nafasi yake katika kupiga kura. Elimu hii huwajengea ufahamu/uelewa wananchi kuhusu haki na wajibu wao kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi wakiwa na taarifa kamili na sahihi juu ya michakato yote ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

Mamlaka ya Tume kutoa Elimu ya Mpiga Kura

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kifungu cha 4C kimeipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, Kuratibu na kusimamia Taasisi, Asasi na watu wanaotaka kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

Kutokana na matakwa ya Sheria iliyotajwa hapo juu, Tume hutoa Elimu ya Mpiga Kura pia kwa kushirikiana ha Asasi za Kiraia katika kutoa Elimu hiyo.

Ushirikiano na Asasi za Kiraia katika utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura

Aidha, Tume imekuwa ikishirikiana na Asasi za kiraia katika kuelimisha umma kuhusu mchakato wa Uchaguzi kwa kutoa Vibali kwa Asasi za kiraia kushiriki kutoa Elimu ya Mpiga Kura. Aidha, Tume ina utaratibu wa kuzialika Asasi hizo zinazokusudia kutoa elimu hiyo ambapo huwasilisha maombi na zana zao za Elimu ya Mpiga Kura ili:

i. Kupitia na kuidhinisha zana na nyenzo zote za Elimu ya Mpiga Kura zitakazotumiwa na Asasi za kiraia na wadau wote wanaojihusisha na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura;

ii. Kupitia na kuidhinisha mipango (program) yote iliyoainishwa na Wadau wa utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura;

iii. Kufuatilia na Kuratibu mpango (program) wa utaoaji wa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhakikisha kwamba zinatolewa kwa umakini, usahihi bila kupotosha Wananchi na zinawafikia walengwa wote waliokusudiwa; na

iv. Kufanya tathmini ya zoezi zima la utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kuona iwapo Elimu hiyo imetolewa ipasavyo na imewafikia walengwa.

Vigezo vinavyotumika katika kutoa vibali ni pamoja na Asasi:-

  1. Kuwa na usajili kwa mujibu wa Sheria za Tanzania;
  2. Kuwa imefanya kazi Tanzania si chini ya miezi 6 toka kusajiliwa;
  3. Miongoni mwa Watendaji wake wakuu, Wawili wanapaswa wawe Watanzania;
  4. Kuwa haina taarifa za kuvuruga amani au kuchochea fujo; na
  5. Kuwa tayari kujigharamia katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

Aidha, Asasi inapowasilisha maombi hayo inatakiwa kuambatanisha:-

  1. Cheti cha Usajili;
  2. Katiba ya Asasi;
  3. Majina ya Viongozi wa juu wa Asasi;
  4. Anuani kamili ya makazi (Physical Address) na Namba za simu za Ofisini na Viongozi;
  5. Zana za Elimu ya Mpiga Kura (Vijarida, Vipeperushi, Mabango, Vipindi vilivyorekodiwa, T-shirt n.k.); na
  6. Ratiba itakayoonyesha tarehe na mahali watakapotoa Elimu ya Mpiga Kura katika halmashauri husika.

Wadau wa Elimu ya Mpiga Kura

Tume imekuwa ikishirikiana na Wadau mbalimbali wa Uchaguzi katika kuhakikisha kila mwananchi anapata Elimu ya Mpiga Kura. Wadau hao ni pamoja na;

  1. Wapiga Kura
  2. Vyama vya Siasa
  3. Asasi za Kidini (FBOs)
  4. Asasi za Kiraia (CSOs)
  5. Vyombo vya Habari
  6. Wanawake
  7. Vijana
  8. Jumuiya za Watu wenye Ulemavu
  9. Taasisi za Serikali
  10. Asasi za Kijamii (CBOs)
  11. Wadau wa Maendeleo
  12. Taasisi za Elimu

Makundi maalum

Ili Elimu ya Mpiga Kura iweze kutolewa na kuleta mafanikio ni muhimu kufanya uchambuzi na kutambua makundi ambayo yanalengwa kupatiwa elimu hiyo. Aidha, nyenzo na Vifaa vitakavyotumika kufikisha ujumbe uliokusudiwa ni muhimu pia kutambuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeyagawa makundi haya maalum katika sehemu kuu nne kama ifuatavyo:

  1. Makundi yaliyojitenga kutokana na sababu za kijiografia;
  2. Makundi yatokanayo na sababu za kimaumbile;
  3. Makundi ya wasiojua kusoma na kuandika;
  4. Wanawake na Vijana

Makundi yanayotokana na sababu za kijiografia na shughuli za kiuchumi

Makundi yanayotokana na sababu za kijiografia ni pamoja na wafugaji, wawindaji na wakulima. Vilevile, makundi haya ni ya watu ambao wanategemea kilimo, ufugaji na uwindaji.

Katika utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kundi hili ni muhimu kuzingatia misimu yao ya kilimo na ufugaji kwa kuwa ni watu wanaohama kutoka eneo moja kwenda lingine kutegemeana na hali ya hewa.

Makundi yatokanayo na sababu za kimaumbile

Makundi haya ni yale yanayojumisha watu wenye ulemavu wa namna mbali mbali kama vile wasioona, wenye ulemavu wa kusikia, walemavu wa ngozi na wenye ulemavu wa viungo.

Makundi haya yanahitaji umakini zaidi katika kuwahudumia kwa kuzingatia maumbile yao, mfano kutumia lughaza alama na nukta nundu.

Makundi ya wasiojua kusoma na kuandika

Kundi hili ni la wapiga kura wasiojua kusoma na kuandika, ili kufikisha ujumbe katika kundi hili ni muhimu kutumia picha na maelezo ili kuweza kuwapa ufahamu kuhusu haki na wajibu wao kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi ili kuwa na taarifa kamili na sahihi za michakato yote ya Uchaguzi.

Wanawake na Vijana

Wanawake na vijana wameanishwa kuwa ni makundi maalumu kutokana na na baadhi ya Wanawake kunyimwa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi kwa kuzuiliwa na waume zao kutokana na mfumo dume. Aidha, Vijana wengi wamekuwa wakizuiliwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uchaguzi na kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani kwa masilahi ya wanasiasa, yote hayo yamefanyika kutokana na uelewa finyu wa haki zao za msingi za kushiriki katika Uchaguzi.

Njia za utoaji Elimu ya Mpiga Kura

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikitekeleza mkakati wa kutoa Elimu ya Mpiga Kura endelevu kwa kutumia njia zifuatazo:

  1. Mikusanyiko rasmi ya watu: Tume inatumia maonyesho ya Sabasaba, Nanenane, Mikutano ya Serikali za Mitaa (ALAT) na wiki ya Vijana kwa kutoa Elimu ya Mpiga Kura ana kwa ana au kuwapatia vijitabu na vipeperushi vyenye kuonyesha aina mbali mbali za michakato ya Uchaguzi.
  2. Mikutano na wadau: Tume inatumia mikutano na wadau mbalimbali katika kutoa elimu, Aidha imekuwa ikiandaa mikutano katika shule mbalimbali za sekondari kwa lengo la kuwaelimisha wapiga kura watarajiwa kuhusu shughuli za Tume na michakato ya Uchaguzi ili kuwahamasisha kushiriki katika michakato ya Uchaguzi.
  3. Vipindi vya redio na Runinga: Tume inaandaa na kutekeleza programu ya kushiriki katika vipindi mbali mbali vya redio na television ili kuweza kuwaelimisha wananchi kuhusu sheria na kanuni mbali mbali za Uchaguzi.
  4. Makala za magazeti: Tume inaandaa makala mbalimbali katika magazeti mbalimbali lengo likiwa ni kutoa habari na kuelimisha umma kuhusu Sheria na taratibu za uendeshaji Uchaguzi.
  5. Mitandao ya kijamii; Tume pia imekuwa ikitumia mitandao ya kijamii katika kutoa habari za kuelimisha na kufahimisha.
  6. Vijitabu, vijarida na vipeperushi: Tume pia imekuwa ikiandaa vijitabu na vijarida mbali mbali ambavyo huvigawa kwa wananchi bure lengo likiwa ni kuwapatia uelewa kuhusu taratibu za Uchaguzi.

Zana za Elimu ya Mpiga Kura

Katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura Tume hutumia zana zifuatazo:

  1. Vijitabu;
  2. Vijarida;
  3. Vipeperushi;
  4. Mabango;
  5. Matangazo ya Runinga na Redio na Magazeti katika kuelimisha wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.