• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DC Magala Afungua Mafunzo ya Matumizi ya Mizani za Kidigitali Kuboresha Ukusanyaji wa Korosho Nanyumbu

Posted on: September 14th, 2024

Na, Lunanilo Ngela

Nanyumbu, Septemba 14, 2024  Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mheshimiwa Christopher Magala, amezindua rasmi mafunzo ya matumizi ya mizani ya kidigitali katika ghala la Naishelo, yakilenga kuongeza uwazi na ufanisi katika mauzo ya korosho kwa msimu wa 2024/2025. Mafunzo haya yamewekwa ili kuhakikisha wakulima wanapata uzito sahihi wa mazao yao na risiti papo hapo, kuboresha mchakato wa upimaji wa korosho.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mheshimiwa Magala alieleza kuwa mizani hizo za kidigitali zitawezesha wakulima kuona uzito halisi wa mazao yao mara moja kupitia tarakimu zinazotolewa na mashine. "Mashine itatoa risiti mara moja kwa kilo zilizopimwa, hatua inayosaidia kuhakikisha usahihi na kujenga imani kwa wakulima katika mchakato mzima wa upimaji," alibainisha Mhe. Magala.

Pamoja na hayo, alisisitiza kwa makarani, makatibu, na wenyeviti wa vyama vya msingi kuhakikisha haki inatendeka na zoezi la ukusanyaji na malipo kwa wakulima linasimamiwa kwa uadilifu. "Ni lazima tuhakikishe uwazi na uadilifu katika kila hatua ili wakulima wasikose haki yao," aliongeza Magala.

Kwa mara ya kwanza, mizani hizi za kidigitali zitatumika katika msimu huu wa korosho, hatua inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ikilinganishwa na mfumo wa jadi wa upimaji. Mheshimiwa Magala pia aliitaka kampuni ya Rotai, wasambazaji wa mizani hizo, kuharakisha usambazaji wa mizani kwenye vituo vyote vinavyotumika kukusanyia korosho ili kufanikisha mchakato huo.

Mizani za kidigitali ni sehemu ya juhudi pana ya kuimarisha kilimo na kukabiliana na changamoto zilizokuwepo, kama vile utofauti wa uzito na ukosefu wa uwazi kwenye upimaji. Mfumo huu mpya unatarajiwa kuongeza imani kwa wakulima, kuongeza uwazi, na kuboresha mapato yao kwa kuondoa changamoto zilizokuwa zinakwamisha mfumo wa upimaji wa awali.

Korosho ni zao muhimu linaloongoza katika kuchangia uchumi wa Wilaya ya Nanyumbu. Kwa kuboresha mchakato wa upimaji na uuzaji wa korosho, matarajio ni kuwa wakulima wataongeza mapato yao na kukuza uchumi wa eneo zima. "Mizani hii ni hatua muhimu itakayowezesha wakulima kupata thamani halisi ya mazao yao," alisema mmoja wa wakulima aliyeshiriki mafunzo hayo.

Viongozi wa vyama vya ushirika na wakulima wameonyesha matumaini makubwa kutokana na maboresho haya, wakiona kuwa yatakuwa na athari chanya kwa uchumi wa wakulima na jamii kwa ujumla.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.