• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DC Machali awavua madaraka Walimu Wakuu 30

Posted on: October 5th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali akizungumza na watumishi  wa Umma waliohudhuria Mkutano uliofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mangaka.


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Moses J. Machali amewavua madaraka Walimu Wakuu thelathini (30) kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao. Maamuzi haya ya Wilaya yamekuja baada ya kupokea Ripoti ya Mthibiti Ubora na Mkaguzi wa Shule Wilaya ya Nanyumbu Bi. Madovena Komba ya kipindi cha Januari - Agosti 2018 ambayo Shule 41 zimekaguliwa kati ya 47 zilizokusudiwa kukaguliwa sawa na 87% ya lengo.

Uongozi wa Wilaya umefanya maamuzi hayo katika mkutano uliofanyika Shule ya Sekondari Mangaka na kuhudhuriwa na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari, watendaji wa vijiji na Kata, Wakuu wa Idara pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya. Ripoti ya Ukaguzi imeonesha kuwa Jumla ya shule 30 kati ya 41 zilizokaguliwa, walimu waliandaa maandalio na maazimio kwa asilimia 23 - 0 tuu huku vipindi vilivyofundishwa vikiwa chini ya asilimia 40. Aidha, Katika Ripoti hiyo zipo baadhi ya Shule ambazo hakukuwa na maandalio wala maazimio yeyote yaani walimu walianda na kuazimia kwa 0%. Ripoti imeonesha idadi kubwa ya walimu wakiripoti shule na kutofundisha wanafunzi jambo linalopelekea Wilaya ya Nanyumbu kufanya vibaya katika Mitihani.

Katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa kwa Shule za Msingi Mwaka 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu ilishika nafasi ya 8 kati ya 9 kimkoa na kushika nafasi ya 180 kati ya 186 Kitaifa. Aidha, katika matokeo ya  Mtihani wa Taifa wa Mwaka 2016 kwa Shule za Msingi, Wilaya ya Nanyumbu ilijikuta ikishika mkia katika ngazi ya Mkoa na kushika nafasi ya 185 Kitaifa kati ya Halmashauri 185.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa alifanya Mkutano na walimu wote wa Shule za Msingi na Sekondari wilayani Nanyumbu siku ya Tarehe 25/Januari/2018 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mangaka. Mheshimiwa Byakanwa pamoja na kusikitishwa na matokeo duni ya wanafunzi alitumia muda mrefu kuwakumbusha walimu na watendaji wote katika sekta ya Elimu juu ya wajibu wao na kuhakikisha kiwango cha Elimu kinainuka. Aidha, Mkuu wa Mkoa alisisitiza walimu kufanya kazi kwa moyo.

Wakuu wa Shule waliovuliwa madaraka na Uongozi wa Wilaya ni kutoka Shule za:- Sengenya, Kilosa, Ndwika, Lumesule, Mburusa, Chikunja II, Holola, Chipuputa B, Chinyanyila, Mara, Masyelele, Magomeni, Mkumbaru, Ulanga, Mtalikachau, Nandete, Nandete B, Nakole, Chivilikiti, Marumba, Mitumbati, Makanya, Nandelu, Kamundi, Mkoromwana, Mehiru, Nawaje, Michiga, Likokona B na Mehiru.

Mkuu wa Wilaya amekemea vikali tabia ya wananchi kuchoma moto misitu huku viongozi wa kijiji wakishindwa kuwachukulia hatua. Mheshimiwa Machali ameagiza walimu kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kutunza mazingira. Katika kikao hicho washiriki wamesisitizwa kuepuka Rushwa, kuwaripoti wahamiaji haramu, kuhakikisha wageni wote katika nyumba za kulala wageni wanajisajili katika daftari, kutii sheria bila shuruti, kutimiza wajibu, kuepuka uzembe kazini, kusimamia usafi wa mazingira, kuhakikisha kila mwanakijiji ana choo ifikapo tarehe 30/10/2018, kujiepusha na biashara haramu ya korosho nje ya utaratibu (Kangomba), kuwabaini wanaowapa ujauzito wanafunzi, kuepuka kukopa katika taasisi zenye riba kubwa na zisizopeleka taarifa zake Idara ya Utumishi.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Ofisi ya Habari juu ya uamuzi wa kuwavua madaraka baadhi ya Wakuu wa Shule wamesema wameridhishwa na hatua hiyo kwani kuna baadhi ya shule walimu hawatimizi wajibu wao.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.