• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DC Machali avionya vyama vya ushirika Nanyumbu

Posted on: September 17th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses J. Machali akizungumza na wananchi wa Kata ya Kilimanihewa wilayani Nanyumbu


Na, Lunanilo L. Ngela

Korosho ni zao kuu la biashara katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Zao hili pia ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara nchini Tanzania. Katika Mikoa hii mitatu ya kusini yaani Mtwara, Lindi na Ruvuma zao hili huitwa "Dhahabu ya Kusini". Aidha, Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Magufuli imehakikisha inatafuta soko la uhakika la Korosho na kuinua maisha wakazi wa mikoa yote inayolima korosho.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu kwa kutambua umuhimu wa zao la korosho kwa maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu na Taifa kwa ujumla ameweka mikakati ya Wilaya yake ya namna ya kuongeza uzalishaji wa korosho ikiwa ni pamoja na kuusimamia kikamilifu mchakato wa manunuzi ya korosho. Mkuu wa Wilaya amefanya mikutano na vyama vya msingi akitoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi wa vyama vya msingi kuhakikisha vinatimiza wajibu wake kikamilifu na kwa uadilifu mkubwa.

Katika Msimu wa Kilimo uliopita wa mwaka 2017/2018 baadhi ya vyama vya msingi havikukamilisha malipo kwa wakulima vikiwemo vyama vya Napacho AMCOS, Kilimanihewa AMCOS, Michiga AMCOS na vingine vingi na kuwaacha wakulima wakiambulia patupu. Wilaya ya Nanyumbu ikishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa iliwakamata viongozi wote waliosababisha wananchi kutolipwa fedha zao. Viongozi hao wa vyama vya ushirika walishughulikiwa na mkono wa sheria ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zao ili kulipa fedha ambazo aidha kwa uzembe au kwa maksudi walizipoteza au kuziiba. Baadhi ya viongozi wa ushirika waliondolewa madarakani.

Wilaya ya Nanyumbu katika msimu mpya wa 2018/2019 imeongeza nguvu katika kuhakikisha wananchi wanapulizia mikorosho kwa wakati, kupanda mikorosho mipya ya kisasa na kuihudumia mikorosho yote iliyotelekezwa kwa muda mrefu. Kuzalisha zaidi korosho kutaongeza pato kwa mwananchi mmoja mmoja na Wilaya itapata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo. Mheshimiwa Machali akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu amesisitiza matumizi mazuri ya fedha ikiwa ni pamoja na wazazi kuwekeza katika Elimu. Mkuu wa Wilaya amelaani tabia ya wazazi kuruhusu wasichana wadogo kuolewa ikiwa ni pamoja na kuwakemea wale wote wanaokatisha masomo ya wanafunzi kwa kuwapa mimba. 

Mkuu wa Wilaya akizungumzia Elimu Wilayani Nanyumbu amewahamasisha wafanyabiashara kuwekeza katika Elimu kwa kufungua shule na vyuo binafsi (Private). Ongezeko la shule na vyuo katika ngazi mbalimbali za masomo ni chachu ya maendeleo kwa jamii yeyote. Wilaya ya Nayumbu inatarajia kuanzisha kidato cha tano ifikapo mwaka 2019 katika michepuo ya Sayansi. Aidha, ujenzi wa miundombinu ya shule kuanzia ngazi ya shule za Msingi mpaka Sekondari unaendelea kwa kasi kubwa. 




Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.