• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DC Machali aviagiza vyama vya ushirika kuzingatia ubora wa korosho

Posted on: October 24th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa vyama vya msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mapema leo Tarehe 24/Octoba/2018


Na, Lunanilo L. Ngela

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Moses Joseph Machali amekutana na viongozi wa vyama vya msingi thelathini na saba (37) vya ushirika wilayani Nanyumbu katika ukumbi wa Halmashauri na kufanya mazungumzo nao ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali ya Serikali. 

Katika kikao hicho, Mhe. Machali amewaagiza viongozi wote wa vyama vya msingi vya ushirika kuhakikisha wanazingatia ubora wa korosho wanazozipokea kutoka kwa wakulima. Mkuu wa Wilaya ameongeza kwa kusema kuwa Wilaya haitasita kuchukua hatua wakati wowote itakapobainika kuwa kuna baadhi ya viongozi wanachukua korosho mbovu au zisizofaa kuingia sokoni na kuharibu taswira ya Wilaya pamoja na Nchi katika soko. Aidha, amewaagiza viongozi wote kuhakikisha msimu wa kilimo 2019/2020 wananunua vifaa/mashine za kupimia ubora wa korosho ili kuepuka usumbufu ambao hujitokeza baada ya korosho kukataliwa katika maghala makuu na kurudishwa kwenye vyama vya msingi zilikotoka.

Mkuu wa Wilaya amekemea pia tabia ya makatibu wa vyama vya msingi kutoandika kiasi chote cha korosho alichouza mkulima, kwa mfano mkulima anaweza kupima korosho zake kilo 785.9 wao wakaandika kilo 785 tu huku pointi ya mbele ikiachwa. Lengo la Serikali ni kuhakikisha Mkulima anapata haki yake yote.

Viongozi wa ushirika wamekumbushwa kutojihusisha na biashara ya korosho nje ya mfumo (kangomba) ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanakuwa makini na kazi yao ili kuleta ufanisi mkubwa katika Msimu huu wa biashara wa mwaka 2018/2019.

Mkuu wa Wilaya akizungumzia soko la korosho amewaambia viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika kuwa Serikali ipo bega kwa bega na wakulima katika kuhakikisha wanapata soko zuri la uhakikika. Aidha, amesema kuwa nia ya Serikali chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha mwananchi anafurahia matunda ya kipato cha jasho lake.

Baadhi ya viongozi walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Salum A. Palango na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nanyumbu Ndg. Hamis H. Dambaya ambao kwa pamoja wamewakumbusha viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika kuwa waadilifu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.