• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DC Machali aufurahisha moyo wa Rais Magufuli

Posted on: August 30th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph Machali (kwenye picha) akifanya usafi katika Kituo cha Afya Michiga


Na, Lunanilo L. Ngela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli hivi karibuni alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania. Lengo la Rais Magufuli ni pamoja na kuziba nafasi zilizokuwa wazi ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya viongozi ili kuharakisha maendeleo ya nchi ya Tanzania katika nyanja mbalimbali. Rais Magufuli ni kiongozi pekee ambaye katika kipindi chake cha uongozi nchini Tanzania amefanikiwa kudhibiti mianya mbalimbali ya ubadhilifu wa mali za umma, uzembe, uvivu wa watumishi wa Serikali,  nidhamu na uwajibikaji. Aidha, ni katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli ambapo Tanzania imefanikiwa kuwashughulikia mapapa wa ndani na nje ya nchi waliojifanya miungu watu huku wakilinyonya jasho la mtanzania.

Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Moses Joseph machali umekuwa faraja jipya kwa wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila Mkuu wa Wilaya. Mheshimiwa Machali katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanikiwa kutafsiri maagizo aliyopewa na Rais Magufuli ya kuhakikisha Nanyumbu inapiga hatua kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinakwenda mpaka vijijini. Mhe, Machali amewaagiza watendaji kuhakikisha kila kijiji zinatengenezwa kombora kwa ajili ya kufyatulia tofari ifikapo kiangazi mwakani ili kuhakikisha zahanati zinajengwa kila kijiji. Aidha, ujenzi huo utaenda sambamba na ujenzi wa shule za msingi katika vijiji visivyokuwa na shule pamoja na sekondari kwa kata zote ambazo hazina sekondari mpaka sasa. "Tutakimbia pamoja" anasema Mkuu wa Wilaya akionesha msisitizo wa namna alivyojipanga na wasaidizi wake katika kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Nanyumbu.

Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa ni lazima mwaka 2019 kidato cha tano kuanza katika mchepuo wa Sayansi ili kuwapatia haki ya kuendelea na masomo wanafunzi wote wanafaulu vizuri kidato cha nne. Akizungumzia Elimu, Mhe. Machali amewaagiza walimu kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na wakaguzi kuhakikisha wanazikagua shule zote. Aidha, Mkuu wa Wilaya amewaagiza Maaafisa Elimu pamoja na kitengo cha Utumishi wa Walimu (TSC) kuhakikisha wanawatendea haki walimu.

Mheshimiwa Machali hutumia asilimia sitini (60%) ya mda wake kuwa vijijini kushughulikia kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Machali amefanikiwa kuumaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji katika kijiji cha Lukula ambako wiki chache zilizopita mifugo 36 iliuwawa. Pamoja na kusuluhisha mgogoro huo Mhe. Machali ameagiza kutengenezwa kwa mpango bora wa matumizi ya ardhi unaoonesha maeneo ya wakulima na wafugaji.

"Nanyumbu inapaswa kuwa salama" anasema Mhe. Machali. Ni marufuku kuharibu mazingira kwa kuchoma misitu. Mkuu wa Wilaya pia ameagiza kuhakikisha kila nyumba inakuwa na choo cha kudumu, kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuwafichuwa wale wote wanaohatarisha amani ya nchi. Mkuu wa Wilaya ameanza ziara ya kutembelea vyama vyote 37 vya msingi huku akitoa maelekezo mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya ununuzi wa korosho kwa msimu wa 2018/2019.  




Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda za Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 July 02, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Kutoka Darasani Hadi Gereji: Binti Mdogo Naishero Sekondari Anayesoma na Kufanya Kazi ya Uchomeleaji

    July 03, 2025
  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.