Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Mariam Khatibu Chaurembo akizungumza na washiriki wa kongamano
Na, Lunanilo Ngela
Akifungua kongamano hilo la “Ushawishi Kuhusu Ushiriki wa Viziwi katika Masuala ya Afya” lililoandaliwa na Chama cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Mtwara na kudhaminiwa na Abilis Foundation, Mkuu wa Wilaya amesema kuwa huduma za afya ni haki ya kila mwanajamii na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa huduma bora za kiafya.
Mheshimiwa Chaurembo amewapongeza CHAVITA kwa kuendesha mafunzo ya siku mbili kwa washiriki yaliyolenga kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya afya ya uzazi pamoja na haki za uzazi kwa wanawake viziwi. Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujikita katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa Mtwara Bi. Farida Selemani amemshukuru Mkuu wa Wilaya na watendaji wengine wilayani Nanyumbu kwa kushiriki kongamano hilo na kuuomba uongozi wa Wilaya kushirikiana bega kwa bega na watu wenye ulemavu ikiwemo viziwi katika masuala mbalimbali mhimu ili kurahisisha upatikanaji wa haki za makundi hayo maalum.
Shughuli zilizofanywa na CHAVITA Nanyumbu katika mradi wa awamu hii ni mafunzo ya siku mbili yahusuyo afya kuanzia tarehe 02 – 03/03/2023 pamoja na kongamano la tarehe 04/03/2023 alisema Mratibu wa Miradi CHAVITA Mkoa Ndg. Kasim Mchindula. Aidha, mratibu huyo aliongeza kuwa matokeo yanayotarajiwa baada ya mafunzo ni pamoja na ushiriki na ushirikishwaji wa viziwi katika msuala mbalimbali yahusuyo afya.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.